Mwanamuziki Ahukumiwa Kifungo cha Miaka Miwili kwa Kutoa Video Inayochochea Ngono

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwanamuziki Ahukumiwa Kifungo cha Miaka Miwili kwa Kutoa Video Inayochochea Ngono
Mwanamuziki Shyma wa nchini Misri amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela ikiwa ni wiki mbili tangu akamatwe kwa kutoa video inayoelezwa kuwa haina maadili.Shirika la Habari la nchi hiyo Al-Ahram linaripoti kuwa mwanamuziki huyo amepatikana na hatia ya kuhamasisha ‘dhambi’ na kuvunja maadili ya nchi hiyo.

Video ya wimbo "I Have Issues" wa mwanamuziki h uyo ulitoka mwezi uliopita na kuzusha sintofahamu kwa madai kuwa umejaa vipande vinavyopingana na maadili na utamaduni wa nchi hiyo.

Shyma mwenye umri wa miaka 21 anaonekana katika video hiyo akiwa amevalia sidiria huku akila ndizi na kundi la wanaume likimshangaa.

Mwongozaji wa video hiyo Mohamed Gamal ametakiwa kulipa faini ya dola za Marekani 560 ambazo ni wastani wa Sh1.2 milioni.

Siku moja kabla ya kuhukumiwa kifungo Shyma aliwaomba radhi mashabiki wake kupitia mtandao wa Facebook akisema hakutegemea video hiyo ingetafsiriwa vibaya kutokana na kile kinachoonekana.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad