Ndugai afunguka kwenda kumuona Lissu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Spika wa Bunge, Mhe.  Job Ndugai amefunguka na kusema atakwenda jijini Nairobi nchini Kenya kumuona Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ambaye anafanyiwa matibabu katika hospitali ya Nairobi nchini Kenya kufuatia kupigwa risasi Septemba 7, 2017.

Job Ndugai amesema hayo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma nyumbani kwake na kusema kuwa watakwenda kumuona Tundu Lissu kwani ni mbunge wao na wao wanampenda sana na kudai kuwa kipindi cha nyuma alishindwa kwenda Kenya kwa kuwa nchi hiyo ilikuwa kwenye uchaguzi na haikuwa na utulivu wa kisiasa ila kwa kuwa saizi imetulia anatarajia kwenda baada ya Christmas kumjulia hali.

"Mimi kama Spika siwezi kwenda na kutoka navyotaka Kenya bali napokwenda kule lazima kuwe na taarifa rasmi za kiserikali na kibunge na ninapokelewa hivyo na ninapopelekwa huko hospitali au wapi napelekwa kwa utaratibu huo ndiyo utaratibu wa nchi kwa nchi. Haiwezekani wao wana mechi kama zile (Uchaguzi) halafu spika nazunguka zunguka Nairobi wanaweza kusema ajenda aliyokuja nayo huyu siyo hii, katika pande hizi mbili Watanzania wamemtuma huyu ana ajenda nyingine kwa hiyo unapokuwa kiongozi lazima ujiongeze" alisema Spika Ndugai

Ndugai aliendelea kueleza kuwa "Haukuwa wakati mzuri kwenda Nairobi, ila kwa kuwa haya mambo yamepita na serikali saizi imekaa sawa sawa basi tusubiri Christmas ipite baada ya hapo mtamuona Spika muda si mrefu akienda kumuona Mbunge wake Nairobi au mahali pengine popote pale, yule ni Mbunge wetu na tunampenda sana na tusingependa asikitike kwa lolote lile" alimalizia Ndugai

Mbunge Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi Septemba 7, 2017 akiwa mjini Dodoma na baadaye kupelekwa nchini Kenya jijini Nairobi kwa matibabu ambapo mpaka sasa yupo huko anaendelea na matibabu.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Soika wetu, Ndugai atakwenda akipata Nafasi kumuangalia Mgonjwa.
    Na hili lisifanye la Siasa. Ni spika amekwenda kumuangalia mmoja wa wagonjwa Mtanzania wanaefanya nae Kazi kama mwakilishi wa Jimbo.
    Haendi kutoa Tamko la Serikali kama mnavyo dhani au alivyo uliza TL, Anakwenda kujulia hali na kumuombea Dua Apone halaka na kumshauli aludi nyumbani na kushiliki katika Ujenzi wa taifa na kuendelea na matibabu kama yanahitajika.
    Sisi wote ni Watanzania na Tuina haki sawa kama alivyo Kingwendu na Godilaki mlinga na Joti hata Salama Jabir na Dkt Shika.
    Udumu uzalendo na wadumu Wazalendo.....Tanzania Kwanza.

    ReplyDelete
  2. wanaanza kujikanyaga na kuona aibu, wametahayari mmoja baada ya mwingine.

    ReplyDelete

Top Post Ad