Rais Nkurunziza kufuata nyayo za Kagame, Aja na mpango wa kusalia madarakani hadi 2034

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza ameanzisha kampeni ya mchakato wa kufanyika kwa kura za maoni kujaribu kubadilisha katiba itakayompa nafasi ya kuongeza mihula mingine miwili baada ya kikomo cha utawala wake  mwaka 2020.

Rais Nkurunziza amesema hayo jana jumanne wakati akihutubia wafuasi wake katika kijiji cha Gitega huku akiwaonya wale wote watakaopinga juhudi zake kwa maneno au kwa vitendo watakuwa wameuvuka mstari mwekundu.

Kampeni hiyo maalumu yenye lengo la kumuweka Nkurunziza hadi mwaka 2017 imeanzishwa baada ya serikali kuzindua juhudi za kuchangisha fedha za maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la AFP taarifa zimeeleza kuwa mpango huo unahusisha kuidhinishwa kwa rasimu ya katiba mpya ambayo itamuwezesha kuwania urais kwa mihula miwili zaidi ya miaka saba kila muhula baada ya kustaafu kwake mwaka 2020.

Viongozi wa upinzani wanaoishi uhamishoni wanasema kura hiyo ya maoni itakuwa kama mazishi kwa muafaka wa utiaji saini wa mkataba wa amani wa mwaka 2000.

Mkataba huo wa amani ulisaidia kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka 13 na kusababisha vifo vya watu 300,000.

Burundi ilitumbukia kwenye mzozo mwingine wa kisiasa mwaka 2015 pale Rais Nkurunziza alipokataa kung’atuka madarakani baada ya kumaliza muhula wake na  kuwania tena urais.

Nkurunziza anakuwa Rais wa Pili Afrika Mashariki kuonesha nia ya kubadili katiba ili apewe muda mwingine wa kuongoza baada ya Rais wa Rwanda, Paul Kagame kufanya hivyo mwaka 2016.

Bongo5
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hasa unaitisha kura ya maoni ya nini? Ama ujinga wa demokrasi ndio hyo hakuna MTU wa kuicontro yaan ni bora utawala dikteta tu MTU akae madarakani kimya kimya akitoka amuweke mkewe na watoto zake mpk bas kuliko kudanganywa na upigaji kura

    ReplyDelete

Top Post Ad