Sina Mpango wa Kuhamia CCM Kama Inavyodaiwa Mitandaoni- Kubenea

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Sina Mpango wa Kuhamia CCM Kama Inavyodaiwa Mitandaoni- Kubenea
Mkurugenzi wa Hali Halisi Publishers Ltd (HHPL) na Mbunge wa jimbo la Ubungo,(Chadema) Saed Kubenea amesema hana mpango wowote wa kuhama Chama chake cha Demokrasia na Maendelea(CHADEMA) na kuhamia CCM kama inavyodaiwa mtandaoni.

Kubenea ameiambia Bongo5 leo, kuwa wananchi wanapaswa kupuuza taarifa hizo kwani yeye ataendelea kuwa Mbunge wa Jimbo la Ubungo kupitia Chama chake.

“Nadhani ni udhaifu wa watu kwasababu kama mtu anaandika taarifa kwamba Mbunge ana hama na aliyeandika taarifa hizo ni Mbunge bila kumuuliza Mbunge mwenzake bila kuwasiliana nae hiyo ni shida me naona is not fair,” amesema Kubenea.

“Wananchi wapuuze taarifa zozote zinazonihusisha mimi na kuondoka Chadema na kujiunga na CCM hizo ni za Uzushi mimi bado ni mwananchama wa Chadema na bado ni Mbunge wa Ubungo na sina mpango huo na sijawahi kuzungumza na mtu yoyote.”
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hahahaha! Alokumwagia tindikali kwa sasa ndio 'boss' wako, uhame uende wapi.......hujipendi...KOSA MOJA HALIMWACHISHI MKE tehetehetehe

    ReplyDelete
  2. Kubenea si useme tu ukweli...
    Ukiwastukizia hapo watakuona Msaliti au umesaliti na kuwa msalitiwa.
    Hata kwa niaba yako mie niko tiyari kwa yale tuliozungumza. Ila nangoja Muda Muafaka.

    ReplyDelete

Top Post Ad