Wanaohama Chama Wachunguzwe Ili Kubaini Ukweli wa Sababu Zao- Peneza

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wanaohama Chama Wachunguzwe Ili Kubaini Ukweli wa Sababu Zao- Penez
Mbunge wa Viti Maalum wa Chadema, Upendo Peneza amesema hana sababu za kuhama chama hicho kikuu cha upinzani nchini huku akiwashangaa wanaochukua uamuzi huo.

Peneza amesema kuhama chama kunasababisha hasara kwa Taifa kwa kuingia katika uchaguzi wa marudio huku akipendekeza uchunguzi ufanyike kwa waliohama ili kubaini ukweli wa sababu wanazozitoa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Desemba 15, Peneza amesema hajafikiria kuhama chama lakini anasikitika watu walioaminiwa na wananchi wakajiuzulu kwa kutoa sababu zisizoeleweka.

“Nimehusishwa mimi kuhama chama changu, sina sababu za kuhama ila ninachotaka ni hawa wanaohama watueleze sababu za kutuingiza katika hasara ya kurudia uchaguzi,” amesema Peneza.

“Sioni sababu ya kwenda kuunga mkono halafu utuingize gharama, yaani furaha zako utuingize sisi gharama, hapana…watueleze sababu zao,” ameongeza

Amesema kuna haja ya kupitia Katiba au kuendeleza mchakato wa Katiba ili kuwazuia kugombea wale wanaojiondoa kwa sababu zisizoeleweka.



Peneza amesema “kama unasema unaunga mkono, useme umewafanyia nini wananchi wako au kuunga mkono kwani lazima uchukue kadi ya chama kingine, Watanzania tunachezewa na watu na huu ni mchezo wa kisiasa unafanyika.”

Akizungumza kwa msisitizo, Peneza amesema “ninapinga haya kwa sababu pesa za wananchi hazitumiki vizuri, tunabana matumizi, tunapinga mafisadi halafu fedha badala ya kwenda katika maendeleo lakini tunakwenda katika uchaguzi.”

“Tusiharibu hela kwa kile wanachosema tunamuunga mkono, kama Rais atajenga daraja la Mwanza kwenda Sengerema, nitampongeza, kama chama changu kitanifukuza haya,” amesema Peneza

“Kiuhalisia shida bado kubwa, mbunge wa Siha angesimama akasema amenijengea shule, ametatua matatizo ya wakulima, ardhi sawa ila hayo hayajatekelezwa unamuungaje mkono.”

Kuhusu kuhusishwa kwake na kuhama, Peneza amesema wakati akigombea alijua kuna CCM yeye aliamua kuwa Chadema ingawa akadokeza kwamba hawezi kusema atakuwa Chadema maisha yote.

“Sisemi maisha yangu kwamba nitakuwa hapa, niliapa Novemba 2015 kuwa mbunge naomna Mungu anisaidie nimalize muda wangu salama na nitimize wajibu wangu niliopewa,” amesema Peneza.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Peneza..... Usipenyeze hoja zisizokuwa na Mashiko....!!!!

    Wewe unadhihirisha Kuchelewa katika kuchukua uamuzi ambao baadae utauchukua.
    Tumekuelewa kuwa Umeridhika na Utendaji wa Awamu ya Tano chini ya CCM.
    Wenzako wameamua Kutoa Ushirikiano mapema iwezekanvyo ndiyo ukaona Wamejiunga bila Kuchelewa na Wewe pia Tunakukaribisha. Siha kwa Dkt Mollel ni moja ya Majimbo yenye Maadili na Bylawa Zao second to Non hapa kwetu. Uchapa kazi wa Mollel na Wazeee wa Baraza has no Comparision.
    Siha tunaijua na Molle na Nia Njema kwa Nchi yake tunaujua. We have no Doubt whatsoever.
    Peneza Karibu kama alivyofanya Tanzania Kwanza.Mh.Mollel kushiriki katika ujenzi wa Tanzania yetu Mpya......Makao Makuu yake DODOMA. Mnakaribishwa na Mkumbuke TANZANIA KWANZA

    ReplyDelete
  2. Peneza..... Usipenyeze hoja zisizokuwa na Mashiko....!!!!

    Wewe unadhihirisha Kuchelewa katika kuchukua uamuzi ambao baadae utauchukua.
    Tumekuelewa kuwa Umeridhika na Utendaji wa Awamu ya Tano chini ya CCM.
    Wenzako wameamua Kutoa Ushirikiano mapema iwezekanvyo ndiyo ukaona Wamejiunga bila Kuchelewa na Wewe pia Tunakukaribisha. Siha kwa Dkt Mollel ni moja ya Majimbo yenye Maadili na Bylawa Zao second to Non hapa kwetu. Uchapa kazi wa Mollel na Wazeee wa Baraza has no Comparision.
    Siha tunaijua na Molle na Nia Njema kwa Nchi yake tunaujua. We have no Doubt whatsoever.
    Peneza Karibu kama alivyofanya Tanzania Kwanza.Mh.Mollel kushiriki katika ujenzi wa Tanzania yetu Mpya......Makao Makuu yake DODOMA. Mnakaribishwa na Mkumbuke TANZANIA KWANZA

    ReplyDelete
  3. Mbona kama sijamuelewa.........anazungumzia wanaohama kutoka chadema kwenda CCM au hata Nyalandu alotoka CCM kwenda chadema nayeye anatia hasara? Hivi ingekuwa hao wabunge wanatoka CCM kwenda chadema angeyasema hayo aloyasema? Mbona alipohama Nyalandu toka CCM kwenda chadema hawakutoa mapovu, au walifikiria 'mchezo' umekwisha.....mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu! Halafu CCM hakuna msemaji ama nene, maana naona chadema kila mtu anasema anapojisia, hadi 'vinuka mkojo' wanathubutu kuitisha press conference kuishambulia CCM eti inawanunua, CCM wapo kimya tu WHY?? au wapo bize na chaguzi......msinyamaze bana, hebu jibuni mapigo, tena mjibu kwa kishindo kile cha kuwachukulia wanachama na viongozi wao ili wachonge vizuri....kudadeki..........piipoooz PWAAAAA

    ReplyDelete
  4. Raha ya mechi wote mtimie sasa naanza kuona upande mmoja watacheza 6 mwingine 11

    ReplyDelete
  5. Raha ya mechi wote mtimie sasa naanza kuona upande mmoja watacheza 6 mwingine 11

    ReplyDelete
  6. Peneza, Sura yako inakusuta... Wewe ni CCM Damu Damu.
    Usione haya Kujitambulisha na kunena ya Rohoni mwako.

    ReplyDelete

Top Post Ad