Ester Bulaya Alia na Fao la Kujitoa...Adai ni Mtaji wa Kujitoa na Umaskini

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Esther Bulaya amesema bado lipo hitaji muhimu la kuwepo fao la kujitoa kwani linaweza kumtoa mwanachama kwenye umaskini wa kipato.

 Mhe. Ester Bulaya ameeleza hayo leo Bungeni wakati alipokuwa anatoa maoni ya kambi hiyo baada ya kuwasilishwa muswada wa sheria ya mfuko wa hifadhi ya jamii kwa watumishi wa umma wa mwaka 2017 ambao umelenga kuunganisha mifuko minne ya umma na kuwa mmoja wa hifadhi ya jamii kwa watumishi wa umma.

"Bado kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na fao la kujitoa kama ilivyokuwa linatolewa na mifuko iliyokuwapo ni la msingi na lazima. Kwani mwanachama anakuwa tayari na akiba yake na hivyo huo unakuwa ni mtaji wa kumtoa kwenye umaskini wa kipato", alisema Bulaya.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama amesema lengo la kuunganishwa kwa mifuko hiyo ya pensheni ambayo ni PSPF, LAPF, GEPF na PPF ni kukidhi kilio cha muda mrefu cha wafanyakazi kuhusu kuunganisha mifuko hiyo ili kupunguza gharama za uendeshaji.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hivi vyeo na Miito hii... Mnajibandikaje?

    "Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Esther Bulaya"

    Je ameajiriwa na Ofisi ya Waziri Mkuu wa Nchi Gani?

    ReplyDelete

Top Post Ad