Majaliwa Apiga 'Stop' Uuzwa Mali za KNCU Amtaka Anna Mwingila Kusitisha Zoezi Hilo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Majaliwa Apiga 'Stop' Uuzwa Mali za KNCU Amtaka Anna Mwingila Kusitisha Zoezi Hilo
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bibi Anna Mghwira asitishe uuzwaji wa mali za Chama cha Ushirika cha Kilimanjaro (KNCU).


Majali ametoa agizo hilo Januari 17, 2018 wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Serengeti, wilayani Tarime.

Hatua hiyo imekuja baada ya KNCU kutangaza kuuza shamba lake kwa ajili ya kuiwezesha benki yake ya KCBL  kutimiza sharti la mtaji la Benku Kuu ya Tanzania (BoT).

Benki hiyo ya KCBL inatakiwa kutimiza sharti la kuwa na mtaji kamili unaotosha wa shilingi bilioni  tano (5) katika kipindi cha miezi sita tangu kutolewa kwa tangazo hilo.

Waziri Mkuu alisema ni marufuku kuuza mali za Ushirika huo, hususan katika kipindi hiki ambacho Serikali inafanya uhakiki wa mali za vyama mbalimbali vya Ushirika nchini.

Alisema Serikali imedhamiria kuimarisha Ushirika nchini na sasa inafanya uhakiki wa mali za vyama vya Ushirika na watakaobainika kuhusika na ubadhilifu watachukuliwa hatua.

Januari 4, 2018 BoT ilizipa miezi sita benki tatu ili ziweze kuongeza kiwango cha mtaji unaohitajika kutokana na matakwa ya kisheria ya kuwa na mtaji kamili wa kutosha.

Benki hizo ni Kilimanjaro Co-Operative Bank Limited, Tanzania Women Banki Plc na Tandahimba Community Bank Limited, zitakaposhindwa kutekeleza agizo zitachukuliwa hatua.

BoT ni itazifutia leseni na kusimamisha shughuli za kibenki chini ya ufilisi, iwapo benki hizo zitashindwa kutekeleza agizo hilo ihadi kufikia Juni 30, 2018.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad