Mrema Akanusha Taarifa za Kifo Alizozushiwa "Ajafa Mtu Hapa”,

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mrema Akanusha Taarifa za Kifo Alizozushiwa "Ajafa Mtu Hapa”,
Mwenyekiti wa Bodi ya Parole nchini na mwanasiasa mkongwe, Agustino Lyatonga Mrema, amekanusha taarifa za kifo ambazo zilianza kusambaa mitandaoni mapema leo.


Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake Sinza jijini Dar es salaam, Mheshimiwa Mrema amesema yeye ni mzima wa afya na hata ugonjwa amabo ulikuwa ukimsumbua kwa miaka mingi ameshapona.

“Afya yangu ni njema ni kweli nilikuwa mgonjwa tangu mwaka 2015, wakati wa kampeni na wakawa wanasema msimchague Mrema ni mgonjwa ni marehemu Mtarajiwa, ila tangu Magufuli kushika urais wake aliahidi serikali itasimamia matibabu yangu, nikapelekwa India na ile kansa iliyokuwa inanisumbua imepona kabisa”, amesema Lyatonga Mrema.

Mrema ameendelea kwa kusema kwamba...”kwa kweli naona mambo yangu ni mazuri hata sura inang'aa, ngozi ile iliyokunjamana haipo tena. Leo asubuhi nimepata taarifa kuwa kuna kikundi kile kile cha 2015 wanataka nife, wanahisi naelekea tena Vunjo kuchukua lile jimbo, lakini nataka kuwaambia mimi sio mgonjwa kansa nimepona, hajafa mtu hapa”, amesema Lyatonga Mrema.

Leo asubuhi kulikuwa na taarifa kuwa mwanasiasa hyo amefariki dunia, kitendo ambachosio mara ya kwanza kutokea kwa kiongozi huyo, ambaye sasa anashikilia wadhifa wa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole nchini.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad