Mrisho Gambo Aanika Siri ya Kilichompeleka Lowasa Ikulu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mrisho Gambo Aanika Siri ya Kilichompeleka Lowasa Ikulu
MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amefunguka na kuweka wazi kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa alikuwa na kiu kubwa ya kukutana na Rais John Pombe Magufuli tangu siku nyingi.



Gambo amesema hayo jana Januari 10, 2018 wakati akiongea na waandishi wa habari na kudai kuwa amefurahishwa kuona kiu hiyo ya Lowassa kukutana na Rais Magufuli imefikiwa pale Ikulu huku akidai kuwa hata wao kama viongozi wameweza kujifunza jambo kutoka kwa Rais Magufuli kukubali majadiliano na kiongozi huyo wa upinzani.



“Ni kweli kwamba Mhe. Lowassa alikuwa na kiu kubwa ya kukutana na Rais na Mtanzania yoyote mwenye akili timamu lazima awe na kiu hiyo ya kumuona Mhe. Rais kwa sababu yeye ndiye Rais wetu Watanzania, yeye ndiye amepewa dhamana kutuletea maendeleo sisi kama taifa kwa hiyo mtu yoyote hata kama si Mtanzania ana jambo lake lolote la kimaendeleo njia nyepesi ya kulifanikisha ni lazima ampitie mtu ambaye amepewa mamlaka na Watanzania.” alisema Mrisho Gambo



Aisha Gambo alitumia nafasi hiyo naye kumpongeza Rais John Pombe Magufuli “Nampongeza Mhe. Rais kwanza kwa kuonesha ajenda yake kubwa ni maendeleo kwamba uchaguzi alishamaliza 2015 sasa hivi anajielekeza kwenye maendeleo, ni Rais ambaye hana ubaguzi ameshakutana na viongozi wengi wa dini, wanasiasa na amekutana na makundi mbalimbali. Rais jana ametufundisha uongozi hasa zaidi sisi viongozi vijana” alisisitiza Gambo.



Januari 9, 2018 kiongozi wa CHADEMA ambaye aligombea nafasi ya Rais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Edward Lowassa alimtembelea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaama na kumpongeza kwa kazi nzuri anazofanya.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad