Mtoto wa Rais Mstaafu Atumbuliwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mtoto wa Rais Mstaafu Atumbuliwa
Rais wa Angola  João Lourenço, amemfukuza kazi mtoto wa rais wa zamani wa nchi hiyo José Eduardo dos Santos ambaye alikuwa Mkuu wa mfuko wa utajiri wa taifa hilo.


Rais  Lourenço alikaririwa akisema kwamba ameamua kumbadilisha José Filomeno dos Santos kufuatia tume ya ndani ya uchunguzi juu ya utawala wa mfuko huo huku kukiwa na taarifa kwamba dola bilioni 5 kutoka katika mfuko huo zimetumika katika hali tete tangu mwaka 2011 mfuko huo ulipoanzishwa.

Awali Novemba 15, Rais huyo alimfukuza kazi binti mkubwa wa rais huo wa zamani, Bi Isabel dos Santos kama mkuu wa kampuni ya mafuta ya serikali ya nchi ya Sonangol.

Aidha Rais huyo amemteuwa Waziri wa Zamani wa Fedha kuwa mwenyekiti wa bodi  ya mfuko huo (FSDEA) Carlos Alberto Lopes.

Mfuko huo umekuwa ukitajwa sana kufuatia tuhuma zilizovujishwa na gazeti la Paradise kwamba ulilipa fedha nyingi mamilioni ya dola ikiwa na malipo ya ada kwa mfanyabiashara ambaye anafanya kazi kwa karibu na José Filomeno.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad