Mwigulu Apiga Stop Utoaji wa Pasipoti za Makundi.

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 Mwigulu Apiga Stop  Utoaji wa Pasipoti  za Makundi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Mwigulu Nchemba amesitisha utoaji wa hati za kusafiria za makundi.

Amesema uamuzi huo unatokana na baadhi ya waombaji wa hati hizo kwa ajili ya kwenda kufanya kazi nje ya nchi kufanyishwa shughuli zingine kinyume cha sheria za nchini.

Dk Nchemba amesema Serikali itaandaa utaratibu mzuri kati ya Tanzania na nchi husika wanakokwenda wahusika ili waandaliwe mazingira mazuri na salama ya kufanyia kazi na kujiridhisha na kile wanachokwenda kufanya.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Januari 25,2018 Dk Nchemba amesema baadhi ya matendo yanayokiuka sheria za nchi wanayofanyiwa ni kazi zisizo na maadili na kuwekwa rehani kutokana na masuala ya dawa za kulevya.

Dk Nchemba pia ameagiza kampuni zinazoingiza makundi ya watu wanaokuja kufanya kazi nchini kuripoti leo kwa  kamishna wa mipaka na vibali.

Agizo hilo amesema linatokana na baadhi ya kampuni hizo kuwatafutia kazi raia wa kigeni na wanapofika nchini hufanya kazi tofauti ikiwemo biashara ya ngono.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad