Nani Anafaa Kupeperusha Bendera ya Chadema 2020?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

LOWASSA ALIWASALITI WENZAKE.

Na Thadei Ole Mushi.

Maana halisi ya chama cha siasa ni kikundi cha watu wenye nia moja na Lengo moja la kushika madaraka ya nchi.

Hii maana imekuwapo karne na karne na ndio msingi na lengo kuu la kuundwa kwa vyama vya siasa.

Hakuna chama cha Siasa duniani ambacho kiliundwa na hakitambui lengo hili kama lengo la msingi

LOWASSA HAFAI TENA KUWA MGOMBEA URAIS KUPITIA UPINZANI.

Huu ni ukweli ulio uchi kuwa kwa kitendo cha Lowassa kujitokeza hadharani na kusifia serikali ya awamu ya Tano moja kwa moja inamvua sifa ya kupeperusha bendera ya Chadema kwenye uchaguzi mkuu

Kitendo alichokifanya hakina Tofauti na wabunge au madiwani walioamua kujivua nafasi zao na kujiunga ccm kwa kisingizio cha kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli.



Lowassa amesema kuwa Rais kafanya mazuri sana katika uongozi wake moja kwa moja kaunga Mkono juhudi za Rais Magufuli sasa huyu unamtofautishaje na Dr Molel? Au kina Mtulia?

Lowassa atapata wapi tena ujasiri wa Kusimama jukwaani na kusema achaguliwe huku yote yaliyofanywa amekubaliana nayo? Litakuwa ni kosa la Kiufundi kweli kama chadema itamchagua tena Lowassa kuwa mgombea Urais 2020.

Huu ni usaliti katika dhana ya maana ya chama cha Siasa kama nilivyoielezea hapo mwanzo.

NINI KINAWEZA KUFANYIKA.
Kwa sasa Chadema inatakiwa ianze kuoiga mahesabu mapya ya nani anauzika kwa wananchi. Kwa upande wao wafikirie majina haya mawili.

1. Fredrick Sumaye.

2. Tundu lisu.

SUMAYE.
Huyu anafaa kwa sifa moja tu kubwa kwamba aliwahi kushika nafasi kubwa ya kiuongoz nchini lakini hakuwahi kuwa mwanasiasa mkubwa.

Kuna tofauti kati ya kuwa mwanasiasa mkubwa na Kiongozi mkubwa. Hii ina maana kuwa Sumaye alidondokewa na bahati ya kupitishwa kuwa waziri mkuu na sio kwamba alikuwa na ushawishi kwa jamii kuipata nafasi hiyo aliyodumu nayo kwa miaka 10.

HASARA YA SUMAYE.
Sumaye kama alivyo Lowassa ni mtu mwenye makando kando mengi. Kama ilivyo kwa viongozi wengi hasa kujilimbikizia Mali.
Sumaye naye amekuwa akitajwa tajwa kama ataanza kujiandaa kwa ajili ya kushika form ya urais basi CCM wanajua pa kugusa ili atulie. Na wakipagusa sana anaweza akahamia kabisa CCM kulinda asife maskini. Huu ndio ukweli wenyewe......
Hawa kina Lowassa wanalinda tu mali zao kwa sasa hawana ubavu tena wa kuzungumza lugha ya kuiondoa ccm madarakan.

LISU.

Huyu pamoja na kuwa ni msomi mzuri, ni mwanaharakati na ni mpinzani haswa haswa. Kwa sifa hizo anatosha sana kupeperusha bendera za Chadema Kwa sasa.

Huyu hakuwahi kushika nafasi kubwa za kiuongozi ila ni mwanasiasa mkubwa sana kwenye ukanda huu wa Africa Mashariki.. angelikuwa CCM huyu ni dhahiri angeliteuliwa kushika nafasi kubwa kabisa za Kiuongozi.

Narudia kama tunataka kuona kampeni zenye mvuto 2020 Lisu ndio chaguo pekee la Chadema. Wakimsimamisha huyu atatusumbua sana CCM.

HASARA YA LISU.
Kipingamizi kikubwa cha Lisu kwa sasa ni Afya yake. Lisu anatakiwa kwa sasa apiganie zaidi Afya yake kuliko kitu kingine kile.
Kipingamizi cha pili cha lisu hana agenda ya msingi ya Kiuchumi ya kumpeleka Ikulu zaidi ya kuwa mkosoaji mkubwa. Lisu anapaswa sasa kuanza kuonyesha Plan B zake katika maswala ya kitaifa yaani kama jambo limefeli yeye kama yeye angelifanyaje.
Naamini na ndivyo ilivyo kiongozi mzuri ni yule mwenye maono yake juu ya mambo flan yaani mawazo yake binafsi na sio ya kuandikiwa (Ilani) na ndio maana hata Rais wetu kuna saa anaweka ilani Pembeni na kunyoosha kwa namna anavyoamini yeye.

Lisu anatakiwa sasa atuonyeshe nje ya Ukosoaji wake nini plan na Dira yake kwa taifa hili.


By Ole Mushi/JF

0712702602


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mgombea Tundu Lisu kuwa na uwezo wa kuja kuisumbua CCM kwenye uchaguzi wa uraisi 20/20? Hivyo ni vichekesho na maneno ya mitaani. Tundu Lisu hata kile kiti chake cha ubunge hawezi kukitetea hivi sasa kama atasimama kugombea . Wema Sepetu anaweza kuwa na mvuto mkubwa zaidi kama atasimama kugombea uraisi kuliko hata Tundu Lisu. Sababu tatu kuu zinazofanya wapinzani wanaongozwa na Chadema hawana haja hata ya kufikiria tiketi ya Lisu kumsimamisha kwa kiti cha uraisi.
    (1) MAKINIKIA.MAKINIKIA. MAKINIKIA. kitendo cha Tundu Lisu kupinga hadharani juhudi zilizokuwa zinachukuliwa na serikali ya Magufuli kuhakikisha Tanzania na watanzania wanapata haki yao na kufaidiika na rasilimal zao kimeaacha makovu ya uchungu yasiyofutika katika nyoyo za watanzania. Kumbuka Tundu Lisu alifikia hata kuitishia na kuionya serikali kwamba iachane na juhudi zile la sivyo itashitakiwa na jumuiya za kimataifa. Tundu Lisu aligeuka kuwa mtetezi wa walowezi wa kigeni.
    (2) Idadi kubwa ya hadhina ya wanachama iliyonayo CCM inayojazwa nyama na watanzania wengi wanaomsapaoti na kumuunga mkono Maghufuli. Kumbuka idadi kubwa ya wanachama wa CCM na watanzania wanaomuunga mkono Maghufili wanamchukulia Tundu Lisu kama muhuni fulani hivi aliekosa adabu.
    (3) Maghufuli.Maghufuli. Maghufuli.
    Maghufuli sio kigingi kwa Lisu tu bali kutoka upinzani wote huwezi kumuona wa kusimama na Maghufuli akamletea bughudha. Edward Lowasa kutokana na msimamo wake wa wastani wa kisiasa anaweza kujaza mikutano miwili mitatu wakati wa kampeni na ni mgombea pekee anaweza kupata idadi kubwa zaidi ya kura kutoka upinzani lakini kura zake haziwezi kufikia idadi ya kura ya uchaguzi uliyopita.
    Upinzani wanatakiwa kuachana na siasa za kiuharakati na kujikita zaidi na siasa za kiuafikiano hasa na mamlaka ili kuendana na page mola ya mtizamo wa kimaendeleo ya nchi badala ya kuendekeza majibizano.

    ReplyDelete

Top Post Ad