Okwi Ajiunga na Kambi ya Simba Morogoro

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Okwi Ajiunga na Simba  Kambini Morogoro

Baada ya kuwepo kwa tetesi nyingi kuhusu mshambuliaji wa Simba Emmanuel Okwi ambaye ni kinara wa mabao kwenye ligi kuu soka Tanzania Bara, hatimaye nyota huyo amejiunga na kambi ya timu hiyo.

Okwi amejiunga na kambi ya timu hiyo mjini Morogoro jana jioni tayari kwa maandalizi ya mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara dhidi ya Singida United utakaopigwa Alhamisi hii kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Taarifa ya klabu ya Simba imeeleza kuwa Okwi ambaye ni raia wa Uganda alisafiri jana akitokea Dar es salaam hadi Morogoro katika Chuo cha Biblia, Bigwa ambako klabu hiyo imeweka kambi.

Okwi amepokelewa na Kaimu kocha mkuu wa Simba Masoud Djuma na kufanya mazoezi leo asubuhi. Okwi anaongoza orodha ya wafungaji akiwa na mabao nane licha ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu.

Okwi aliumia mapema mwezi Novemba hivyo kukosa mechi kadhaa za ligi kuu ikiwemo michezo miwili ya jijini Mbeya ambapo Simba ilicheza na Tanzania Prisons pamoja na Mbeya City na mchezo wa raundi ya 12 dhidi ya Ndanda FC.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad