Zitto Kabwe Azuiliwa Kufanya Mkutano na Polisi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Zitto Kabwe Azuiliwa na Polisi
Jeshi la Polisi Kigoma limemzuia Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe kufanya mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Uwanja wa Mwanga Community Center, mkoani Kigoma ambao ulipaswa kufanyika leo Januari 16, 2018.


Taarifa iliyotolewa na OCD inasema kuwa kiongozi huyo hakufuata utaratibu wa kutoa taarifa ndani ya masaa 48 kabla ya kufanyika kwa mkutano huo jambo ambalo Mbunge Zitto Kabwe amelilamikia na kusema kuwa amezuiwa kufanya Mkutano kinyume na sheria ya Bunge ya mwaka 1988.

"Mimi sitaki kuwapa polisi sifa ya kupambana nasi. Tumeahirisha mkutano mpaka siku ya jumamosi Lakini tumewaandikia barua rasmi kuwa sheria waliyonukuu sio sheria halali na haihusiani na mikutano ya Mbunge kwenye jimbo lake la Uchaguzi. Sheria wanayopaswa kunukuu ni sheria namba 3 ya mwaka 1988 kifungu cha 4(1)". Alisema Zitto Kabwe

Kufuatia jambo hilo Zitto Kabwe amedai kuwa atamwandikia barua rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai kuhusu suala hilo ili kutengeneza mazingira kwa siku za usoni lisije kumtokea Mbunge mwingine yoyote.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Polisi wanasheria, serikali inasheria , bunge linasheria. Ukweli ni kwamba hakuna sheria na watu hawazijui sheri zao.kila mtu analeta sheria zake mwenyewe. Na sheria hizihizi hazitumiki vyema wala sawa. Ni mfumo mbovu kiuongozi. Viongozi wengi wanachukulia sheria mikononi na ni hatari.

    ReplyDelete
  2. Zitto zumbli kambwe... Sasa amekuwa ni mwanashelia. Maalufu kati Aflika ya mashaliki na kati.
    Zito zumbli kabwe atamuandukia balua spika Job Ndugai kumweleza na kufundisha shelia.
    Dogo anajikita sasa Ujiji kuwafanyia mikutano na kupoteza boya wana Kigoma na Muda waopia.
    HATUTAKI UKANYABOYA ZITTO. LUDI MJJINI ULIKOHAMIA.

    ReplyDelete

Top Post Ad