Familia Yenye Utata ya Gupta Mwenye Mahusiano ya Karibu na Rais Jacob Zuma Yavamiwa na Polisi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 Familia Yenye Utata ya Gupta Mwenye  Mahusiano ya Karibu na Rais Jacob Zuma Yavamiwa na Polisi
Askari Polisi mjini Johannesburg nchini Afrika Kusini wameizingira nyumba ya familia ya kitajiri ya ‘Gupta’ ambayo ipo na mahusiano ya karibu na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma.

Picha inayohusiana
Rais Jacob Zuma akiwa na baadhi ya wanafamilia ya kifahari ya GUPTA.

Kwa mujibu wa mtandao wa Reuters umedai kuwa polisi wamezingira barabara zote zinazoingia kwenye eneo la nyumba za familia hiyo huku wakiwa na silaha nzito za kijeshi.

Msemaji wa jeshi la polisi mjini  Johannesburg, Hangwani Mulaudzi amethibitisha taarifa hiza lakini amekataa kutolea maelezo kwa nini nyumba hiyo ya kifahari imezingirwa na polisi.

Tangu mwaka 20015 familia ya Gupta imekuwa ikishutumiwa na viongozi wa upinzani nchini Afrika Kusini kuwa inahifadhi mali za wizi zinazoibwa serikalini na Rais Zuma.

Ulinzi huo umekuja katika kipindi hiki ambacho Chama cha ANC kwa sauti moja kimetoa tamko la kumshinikiza Rais Jacob Zuma kujiuzulu nafasi yake ya urais.

Jana chama hicho kilimpa masaa 48 Rais Jacob Zuma kujiuzulu urais huku mwenyewe akitaka apewe muda wa miezi mitatu hadi sita kuchukua uamuzi huo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad