Klabu ya Simba: Okwi Yuko Fiti Leo Ataungana na Wenzake Kwenye Mazoezi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Klabu ya Simba:  Okwi Yuko Fiti Leo Ataungana na Wenzake Kwenye Mazoezi
Uongozi wa Klabu ya Simba umesema hali ya mchezaji wao Emmanuel Okwi unaendelea vizuri huku wakidai kuwa jioni ya leo ataungana na wenzake kufanya mazoezi katika uwanja wa Boko Jijini Dar es Salaam.

Tarifa hiyo imekuja baada ya mchezaji huyo jana (Jumapili) kushindwa kumaliza mchezo dhidi ya Ruvu Shooting kutokana na kupata majeruhi kwenye shingo yake kwa kuchezewa ndivyo sivyo na mchezaji Mau Bodi.

Mbali na hilo, Emmanuel Okwi mpaka sasa ndio anayeongoza kwa ufungaji wa magoli kwa kupata 12 akifuatiwa na John Boco kwa mabao 9, nafasi ya tatu kushikwa na Habibu Kiyombo kutokea Mbao FC kwa magoli  8 huku wapinzani wao wajadi wakiwa nafasi ya tano kwa kuwakilishwa na Obrey Chirwa kwa magoli 7 pekee katika msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2018.

Kwa upande mwingine, timu ya Simba SC inatarajia kukichapa na Azam FC siku ya Jumatano (Februari 7, 2018) katika dimba la Taifa.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad