Lissu Atembelewa na Maofisa wa EU

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Lissu Atembelewa na Maofisa wa EU
Maofisa watatu wa Jumuiya ya Ulaya (EU) leo Februari 5,2018 wamemtembelea Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu anayeendelea na matibabu nchini Ubelgiji.

Lissu alishambuliwa kwa zaidi ya risasi 30, Septemba 7 mwaka jana na kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na siku hiyohiyo alihamishiwa Hospitali ya Nairobi alilazwa hadi Januari 6,2018  alipohamishiwa Ubelgiji katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven, anakoendelea na matibabu.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa leo Februari 5,2018 Lissu amewataja maofisa hao kuwa ni Mkuu wa Idara ya Pembe ya Afrika na Afrika Mashariki katika Wizara ya Nje ya EU, Patrick Simonnet.

Wengine ni Mkuu wa Dawati la Tanzania katika EU, Marta Szilagyi, Vania Bonalbert ambaye ni ofisa wa ubalozi wa EU Tanzania anayeshughulikia masuala ya utawala bora na haki za binadamu na Hortensia May Lyatuu.

Amesema ujumbe wa maofisa hao mbali ya kumjulia hali walifanya mazungumzo ya masuala mbali mbali yanayohusu Tanzania.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad