Mbowe Amshtumu Mkuu wa Mkoa wa Mbea Kuhusika Katika Kifungo cha Sugu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mbowe Amshtumu Mkuu wa Mkoa wa Mbea Kuhusika Katika Kifungo cha Sugu

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe. Freeman Mbowe amedai kuwa hukumu ya kesi ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘SUGU’ ilipangwa hotelini siku 4  kabla ya mahakama kutoa hukumu.

Mhe. Mbowe amesema kuwa suala hilo lilipangwa na hata Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amosi Makala alilijua hilo kuwa SUGU atafungwa huku akimtuhumu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amosi Makala kuhusika.

“Hukumu ya SUGU ilifahamika na ilipangwa hotelini, kwamba Sugu anafungwa miezi mitano tulipata taarifa hizo siku 4 kabla. Na kwamba polisi walikusanywa mkoa mzima wa Mbeya, Mkoa mzima wa Songwe, watu wa usalama wa taifa wakajazwa Mbeya kukabiliana na presha ya wananchi ni jambo liliratibiwa. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya anauhusika na anajua jambo hili, Amosi Makala,”amesema Mhe. Mbowe leo Jumanne kwenye mkutano wake na Waandishi wa Habari uliofanyika katika Ofisi za makao makuu Jijini Dar es salaam .

Kwa upande mwingine Mhe. Mbowe amesema kuwa CHADEMA hawaingilii maamuzi ya mahakama bali wanawasema baadhi ya watendaji wa mahakama wanaotumika kisiasa.

“Tunaiheshimu sana mahakama, Muhimili wa mahakama ndio muhimili ambao unasaidia wa Kuregulate nchi, lakini mahakimu mmoja mmoja wanapotumika ndio wanaichafua mahakama na wanalichafua taifa,“amesema Mbowe.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad