Ndugu Wagoma Kuchukua Mwili wa Akwilina

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 Ndugu Wagoma Kuchukua Mwili wa Akwilina
Dada wa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline aliyeuawa kwa kupigwa risasi na polisi, Tegolena Uiso amesema hawatapokea mwili wa mwanafunzi huyo bila kuelezwa nini kilichomuua ndugu yao.

Mwili wa Akwilina umehamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ukitokea Hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi.

Akizungumza leo Februari 19, 2018 na MCL Digital akiwa MNH, Tegolena amesema ni vyema wakapewa ripoti kuhusu kilichogundulika baada ya ndugu kuelezwa kuwa mochuari ya  Muhimbili kwamba watatoa ripoti ya uchunguzi baada ya siku 14.

"Sisi tumekuja kwa ajili ya kujua hasa ndugu yetu nini kimemkuta hatuwezi kupokea mwili bila ripoti. Wanatuambia  ni baada ya wiki mbili sina hakika kama hawajabaini kitu chochote, hatuwezi kuuchukua mwili mpaka tupewe sababu," amesema Tegolena.

Amesema mpaka sasa wamezungumza na Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji NIT, Profesa Zakaria Mhanilwa ambaye bado anawasiliana na madaktari ndani na hawajajua iwapo atakuja na majibu sahihi.

Awali, Profesa Mhanilwa amesema amefika hospitalini hapo kufuatilia uchunguzi huo akiwa ni miongoni mwa wafiwa.

Akwilina alifariki dunia Februari 16, 2018 baada ya kupigwa risasi kichwani akiwa kwenye daladala wakati polisi wakiwatawanya waandamani ambao ni wafuasi wa Chadema.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad