NEC Yamjibu Mbowe Yamtaka Akasome "Hapaswi Kiongozi Kama Yeye"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

NEC Yamjibu Mbowe Yamtaka Akasome "Hapaswi Kiongozi Kama Yeye"
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imefunguka na kudai malalamiko yaliyotolewa jana (Jumanne) na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe sio ya kweli bali yamejaa upotoshaji wa hali juu ambao haupaswi kufanywa na kiongozi kama yeye.


Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa tume hiyo, Kailima Ramadhani baada ya kupita siku moja tokea Mhe. Mbowe kuzungumza mbele ya waandishi wa habari kuwa Tume ya Uchaguzi iliwafanyia hujuma katika kutoka viapo vya Mawakala wao kwenye chaguzi ndogo za marudio Jimbo la Kinondoni na mambo mengine.

"Tume ya Taifa ya Uchaguzi haijibu malalamiko kwa matakwa ya mtu anavyotaka kujibiwa bali inajibu hoja kwa mujibu wa matakwa ya Katiba, Sheria, Kanunu na maadili ya uchaguzi na maelekezo yote ambayo yapo kwa mujibu wa sheria. Kama majibu ya tume hayakuwafurahisha CHADEMA, tume inasisitiza kuwa walijibiwa kwa matakwa ya sheria na katiba sio matakwa ya Mkurugenzi wa uchaguzi, Tume, Chadema au chama chochote cha siasa",   amesema Kailima.

Aidha, Mkurugenzi Kailima amesema Kanuni, Sheria, maelekezo na maadili ya uchaguzi yameweka utaratibu wa kushughulikia malalamiko na changamoto zinazotokea wakati wa uteuzi, kampeni ambako kuna kamati za maadili na jinsi ya kukata rufaa.

"Kwa masikitiko CHADEMA walitekeleza hatua moja tu katika vipengele hivyo wakati wa uchaguzi, kipengele walichotekeleza ni pale baadhi ya wagombea wao walipoenguliwa kugombea ndipo walifuata utaratibu kwa kuwasilisha rufaa kwa Tume ya Uchaguzi na tume ilipitia na ikawarudishia wagombea wao kwenda kugombea", amesisitiza Kailima.

Mkurugenzi Kailima ameendelea kufafanua

"CHADEMA walitaka wakati wa kampeni, Tume ifanye maamuzi kinyume cha maadili waliyoyasaini. Wakati wa kampeni kuna kamati za maadili ngazi ya jimbo ambayo mwenyekiti ni msimamizi wa uchaguzi na wajumbe ni kutokea vyama vyote vilivyosimamisha wagombea na ndio wanaofanya uamuzi. Chadema waliwasilisha malalamiko kwa tume badala ya kuwasilisha kwenye kamati hizo za maadili zinazosimamia malalamiko yote".

Kwa upande mwingine, Mkurugenzi wa Uchaguzi Kailima Ramadhani amemsihi Mbowe na chama chake wasome sheria za uchaguzi na kuzielewa na kumsisitizia kuwa tume ipo tayari kumpa elimu ya mpiga kura na kuzifahamu sheria hizo zake kwa mapana.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hata ikiletwa hiyo katiba mpya si kwa Mbowe na genge lake wao wapo katika kupinga tu ni kama vile kuna laana fulani inawatafuna. Kwani katiba mpya haiwezi kujisimamia wenyewe ni lazima kuwe na watu waadilifu wa kuisamamia na piga ua mpende usimpende kwa Tanzania tunapozungumzia uadilifu miongoni mwa viongozi basi hakuna kama Magufuli. Sasa utaona Mbowe na genge lake kila kukicha wanaojaribu kuzua kila balaa nchini hadi nje za nchi kujaribu kuwaaminisha watu kuwa Magufuli na serikali yake haifai. Kama nilivyosema hapo mwanzoni kuwa Mbowe na genge lake kama vile kuna laana fulani inawatafuna wasijue nini kinachowamaliza kwa sababu wamekuwa viziwi hawasikii tena na wamekuwa vipofu hawoni tena kwani kama kuna kitu kinachouuwa upinzani hivi sasa Tanzania ni mikakati yao kuamua kupambana na Magufuli personal. Na CCM wanachekelea kwa sababu wamerahisishiwa kazi na wapinzani. Ni rahisi kusema CCM vibaya watanzania wakakuelewa lakini sio Magufuli. Na ukitaka kujua jinsi gani CCM walivyo na confidence hivi sasa angalia katika chaguzi ndogo zilizopita Magufuli hakushiriki wala kutoa kauli yake katika campeni yeyote ile ya uchaguzi kwani alikuwa hana haja ya kufanya hivyo alijua watashinda tu si kwa nguvu ya CCM bali kwa udhaifu wa upinzani. Watanzania wanamkubali na kumuamini mno Magufuli kutokana na sifa aliyojijengea mapema tu katika maisha yake yaliotukuka ya utumishi serikalini kabla hata hajawa raisi. Lakini kwa muda mchache tangu akalie kiti cha uraisi tayari amefanya mambo makubwa kupita matarajio ya watanzania. Sasa atokezee mtu kama Lema au Sugu kwenda kudiriki kumchafua au kumchamba Magufuli kwa kweli ni vichekesho kwa watanzania na zaidi ni kuzidi kuunanga upinzani kuwa una watu vichaa zaidi wanaofaa kukimbiwa. Hata Mbowe ambae hana historia ilio ya wazi katika maisha yeke ya utumishi au hata ule msimamo wake katika shughuli zake za kisiasa ni za kujizonga zaidi ni hatari zaidi pale anapojaribu kuelekeza makombora yake kwa Magufuli ni sawa na kwenda kuirushia mawe nyumba ya concrete wakati nyumba yako ni ya vioo vitupu. La msingi upinzani utaendelea kujimaliza nchini hadi kufa kabisa si kwa hujuma za CCM wala Magufuli bali kwa maamuzi ya upinzani kuamua kupambana na Magufuli binafsi watanzania waliowengi hawawezi kuwaelewa watawakimbia tu.

    ReplyDelete

Top Post Ad