Polisi Yatoa Sababu za Mauaji ya Kikatili ya Diwani wa Chadema

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Polisi Yatoa Sababu za Mauaji ya Kikatili ya Diwani wa Chadema
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Urich Matei amefunguka na kusema kuwa kifo cha Diwani wa Kata ya Nawala tarafa ya Ifakara wilayani Kilombero, Godfrey Joackim (CHADEMA) aliyefariki kwa kupigwa mapanga huenda ni kisasi.


Matei amesema kuwa kiongozi huyo kuna wakati aliwahi kuwaambia wanakijiji kuwa mtu ambaye alikuwa anafahamika kwa jina la Kenani Haule ndiye alikuwa anawasaliti hivyo baada ya muda mtu huyo aliuliwa kwa kupingwa mapanga.

"Mwanzoni mwa mwaka 2016 watu wa Nawawala walikuwa na ugomvi kati ya wanakijiji na bodi ya sukari akiwa diwani wa eneo lile alisimamia wananchi wale kudai lile shamba, kuna kesi ambayo ipo mahakamani mpaka sasa inaendelea lakini aliwaambia mtu mmoja anaitwa Kenani Haule ndiye tatizo, kwa hiyo diwani Godfrey Joackim aliwaambia tu kuwa huyo Haule ndiye anawasaliti hivyo aliwaambia hata kama Kenani akifariki basi wao watakuwa na uwezo wa kupata shamba na kweli muda mfupi Kenani Haule aliuawa kwa kukatwa katwa mapanga tukio ambalo lilitokea kama lilivyotokea kwake, kimsingi kabisa tunaamini Godfrey Joackim atakuwa ameuawa kwa ajili ya kisasi baada ya kifo cha Kenani Haule" alisema Matei

Aidha Kamanda Matei amedai kuwa jeshi la polisi bado linaendelea na uchunguzi na msako mkali unaendelea na kudai hilo ni tukio baya kutokea Morogoro kwa sababu wamempoteza kiongozi wa wananchi wa Nawala na kuwataka wananchi yoyote ambaye anataarifa juu ya mazingira ya mauaji hayo awape taarifa jeshi la polisi ili waweze kuzifanyia kazi zaidi.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad