AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA
Akisoma mashtaka hayo leo Februari 26, 2018, wakili wa Serikali, Godfrey Ngwijo amesema raia hao wanakabiliwa na shtaka la kuingia nchini kinyume na kifungu cha sheria namba 45(i) kifungu (1) ,(2) kilichofanyiwa marekebisho 2016.
Ngwijo amesema Februari 23, 2018 saa moja jioni katika kijiji cha Mazombe wilayani Kilolo, wahamiaji 83 wasio na vibali walikamatwa na kufikishwa kituo cha polisi kwa kuingia nchini kinyume na sheria ambapo dereva wa lori walilopanda hakupatikana baada ya kukimbia.
Amesema wahamiaji hao walikamatwa wakiwa katika hali mbaya kutokana na kukaa sehemu ya nyuma ya lori hilo ambako hakuna hewa ya kutosha, joto kali na kutokula chakula kwa muda mrefu.
Baadhi ya wahamiaji hao leo wamefikishwa hospitali ya mkoa kupata matibabu.
Wakili huyo amesema kati ya waliofika mahakamani kusomewa mashtaka yao, watatu walishindwa kufika kwa sababu bado wako hospitali wanaendelea na matibabu.
Mtanzania aliyekutwa katika gari hiyo, Hassan Mwalusanjo akituhumiwa kusafirisha wahamiaji hao kwa kutumia lori mali ya Gabriel Mwakyambiki mkazi wa Tukuyu kinyume na sheria, alikana kosa hilo.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, David Ngonyani ameahirisha kesi hiyo hadi Machi 2, 2018.
Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu
Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:
NAFASI ZA AJIRA
JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA
GOODLUCK