Tanesco Yawasaka Wezi wa Umeme

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Tanesco Yawasaka Wezi wa Umeme
Shirika la Umeme Tanzania TANESCO Kupitia kikosi kazi maalum limeendesha kampeni kabambe ya kubaini na kutokomeza matukio ya wizi wa umeme pamoja na uhujumu miundombinu ya Shirika Mkoani Njombe ikiwa ni mwendelezo wa jitihada endelevu za TANESCO katika kudhibiti upotevu wa mapato ya Shirika.



Akiongea katika kampeni hiyo, Kaimu Meneja wa TANESCO Makao Makuu anayesimamia Wateja Wakubwa Mhandisi Fredrick Njavike ambaye pia ameongoza Zoezi hilo alisema kuwa, ndani ya siku tano kupitia kampeni hiyo tayari wamekagua takribani wateja 2000 katika Wilaya ya makambako pekee huku Njombe Mjini wakitarajia kukagua wateja 1000.

Njavike ameongeza kuwa katika idadi ya wateja waliokaguliwa, wateja kadhaa walibainika kujihusisha na vitendo vya wizi wa Umeme. Kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama Mkoa wa Njombe wahalifu hao walichukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kulipa gharama za kiasi chote cha umeme walichokuwa wakiliibia Shirika baada ya kupigiwa mahesabu.

"Zoezi hili la ukaguzi na msako wa wezi wa umeme ni zoezi endelevu linalofanyika Nchi nzima na niwatahadharishe wale wote wanaojihusisha na vitendo hivyo kuacha mara moja, kwani ni lazma watagundulika na hatua kali za kisheria dhidi yao zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na malipo ya fidia ya kiasi cha umeme walicholiibia Shirika.

Hivyo niwaombe Wananchi kuendelea kutupa ushirikiano kwa kufichua watu wenye viashiria vya Wizi wa Umeme. Lakini pia niwaombe wateja wetu kutoa taarifa TANESCO pale wanapona hitilafu zozote katika mita zao pamoja na kuepukana na vishoka wanaowashawishi waibe umeme kwani kupitia msako huu hakuna atakayeiba Umeme na akasalimika bila kukuamatwa na kuchukuliwa hatua" Alisema Mhandisi Njavike
Naye Meneja wa TANESCO Mkoa wa Njombe, Mhandisi Emmanuel Kachewa ametoa Wito kwa Wananchi wa Mkoa wa Njombe kuendelea kushirikiana na TANESCO katika kuwafichua wezi wa Umeme popote walipo ili waweze kuchukuliwa hatua na kuokoa upotevu wa mapato ya Shirika kwa ujumla.

Kwa upande wa baadhi ya wananchi walioshuhudia msako huu ukifanyika mitaani waliipongeza TANESCO kwa kuanza kutambua thamani ya mali zao na kulinda umeme wao ambapo mwanchi mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Mponzi alisema kuwa Matukio ya wizi wa umeme yapo mtaani na wakati mwingine yamekuwa yakisababisha hata vifo kwa wahusika kunaswa na umeme wakati wakijaribu kuiba umeme hivyo ni vyema TANESCO pia Wakatoa na Elimu juu ya madhara ya Wizi wa umeme kwa wananchi wote wafahamu.

Aidha TANESCO imekuwa ikiingia hasara kutokana na vitendo vya wateja wachache ambao kwa makusudi kabisa wamekuwa wakiliibia Shirika umeme kwa katika maeneo mbalimbali na hivyo kulikosesha Shirika mapato stahiki na kurudisha nyuma jitihada za TANESCO na Serikali Katika kusambaza Umeme Nchi nzima na hivyo kufifisha kasi ya Uimarishaji wa Miundombinu ya Uzalishaji, Ufuaji na Usambazaji umeme Nchini.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mashirika yote ya umeme Duniani ni miongoni mwa taasisi tajiri sana. Ni umeme unaotumika 24/7 usiku na mchana na kila unapotumika unaingiza pesa na ndio maana nchi zilizoendelea huwezi kuona habari za kukatika umeme hovyo kwani hakuna sababu ya umeme kukatika labda katika matatizo ya mabadiliko ya nguvu za maumbile ya ghalfla yasiotarajiwa. Lakini umeme ni biashara inayojitegemea kujiendesha na kuendesha biashara nyengine kwa faida. Kusikia shirika la umeme linahitaji msaada ili kujiendesha ni vichekesho na fedheha. Sawa na kudai msaada wa kujiendesha kwa Mgodi wa dhahabu unatoa dhahabu? Kuna mambo mengine wacha wazungu watuone ni sisi waafrica ni watu wa hovyo. Miaka nenda rudi eti utasikia kuna mgao wa umeme kwa sababu maji yamengua ziwani? Ni uzembe, kwani maji kupungua ziwani au katika vyazo cha maji ni vitu vinavyojulikana kutokea miezi kadhaa kabla ya tukio. Je hakuna vichwa venye uwezo wa kufikiria jinsi gani ya kukabiliana na tatizo linalojirejea kila siku miaka nenda miaka rudi ? Utaona tatizo sio upungufu wa maji bali tatizo upungufu wa uwezo wa kiutendaji wa watumishi wa mashirika yetu aidha kutokana na ufisadi wa ufuatiliaji na udhibiti wa mapato utakaowezesha shirika kujigharamia katika kuboresha huduma bora zaidi au kuwepo kwa watumishi wasiokidhi uwezo kiutendaji ambao mara nyingi huajiriwa katika misingi ya kujuana ya kindugu kuliko uwezo wa kazi. Hata gharama za kufadhili mradi mkubwa wa umeme wa stiglers Gorge serikali isingepaswa kuhangaika kupata fedha za mradi ule kama Tanesco ingekuwepo katika baadhi ya nchi fulani kwani imeshakuwepo kwa miaka mingi ingetosha kugharimia miradi mingine ya umeme nchini. Ningeishauri serikali ya awamu ya tano kama inataka kuepukana na fedheha ya umeme katika kila siku na kufikia malengo ya uchumi wa viwanda ni lazima wafanye mchakato wa kutafuta na kuwaajiri wataalamu wa kigeni wenye uzowefu katika masuala ya uendeshaji na uzidhishaji wa umeme wa uhakika kwa njia ya faida. Isiwe wataalamu walioopatikana kwa njia ya misaada bali waliotafutwa na serikali na kujiridhisha uwezo wao na kuingia nao mikataba japo kwa kipindi cha mpito halafu wapime mafanikio la sivyo hata ikiwepo hiyo stiglers Gorge tunaweza tukajikuta katika matatizo yale yake.

    ReplyDelete

Top Post Ad