Waziri Atoa Wiki Mbili Mgodi wa Nyakavanglaa Ufunguliwe

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Waziri Atoa Wiki Mbili  Mgodi wa Nyakavanglaa Ufunguliwe
Leo February 20, 2018 stori nayokusogezea ni kuhusu agizo alilolitoa Naibu Waziri Wa wizara ya Madini Doto Mashaka Biteko ameagiza kufunguliwa mgodi wa Nyakavanglaa ndani ya wiki mbili uliopo katika Kata ya Malengamakali Wilaya na Mkoa Wa Iringa ili kuwarahisishia huduma wachimbaji wadogo za kujiingizia kipato chao.

Biteko ameyasema hayo February 19, 2018 wakati akizungumza na wachimbaji wadogo kwenye mkutano wa hadhara mara baada ya kuwasili mgodini hapo kukagua hatua za kiusalama zilizofikiwa tangu kufungwa kwa mgodi huo February 12, 2018 kufuatia matukio matatu ya ajali ambayo yalipelekea vifo vya wachimbaji wanne.

“Jichungeni na kujilinda wenyewe ili kila kinachopatikana serikali ijue imepata kiasi gani na wachimbaji wameingiza kiasi gani na kisemwe hadharani, ndugu zangu Rais anahangaika kuona kila eneo ambalo lina wachimbaji wadogo wana rasimishwa na hatimaye wananufaika na madini yao,”  -Biteko

“Mimi nataka niwaambieni wale wote wanaofikiri katika serikali hii inayoongozwa na Rais Magufuli wanaweza kupenya na dhahabu watafute jambo jingine la kufanya maana jambo hilo limepitwa na wakati” -Biteko
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad