Yanga Yawatoa Hofu Mashabiki Wake "Tutashinda Hata Bila ya Kuwa na Chirwa"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kocha wa Yanga Awatoa Hofu Mashabiki Wake "Tutashinda Hata Bila ya Kuwa na Chirwa"
KIKOSI cha Yanga, kimeondoka jana asub­uhi kwenda Shelisheli kwa ajili ya mechi yake ya marudiano ya Ligi ya Mab­ingwa Afrika dhidi ya St Louis.

Hata hivyo, Yanga im­eondoka nchini bila kuwa na mshambuliaji wake wa kutumainiwa, Mzam­bia, Obrey Chirwa, kwa kile kilichodaiwa kuwa ni majeruhi. Inadaiwa ana maumivu ya misuli.

Hata hivyo, Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa, ame­watoa hofu wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kuwa, watashinda mechi hiyo hata bila ya kuwa na Chirwa.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Nsa­jigwa alisema kuwa wameji­panga kuhakikisha wanafanya vizuri katika mechi hiyo kwa hiyo anaamini kwa wachezaji walioondoka nao, wataiongoza timu hiyo kupata ushindi.

“Watu wengi walishitushwa na taarifa za Chirwa kutoku­wepo katika mechi yetu ya marudiano na St Louis, la­kini wanapaswa kujua kuwa mchezaji huyo siyo pekee ambaye hucheza uwanjani.



“Kwa hiyo, kuna mchezaji ambaye tumemwandaa ili kuziba nafasi hiyo na tunaamini atafanya vizuri, niwaombe tu wapenzi na mashabiki wetu kutokuwa na hofu na hilo, tutafanya vizuri,” alisema Nsajigwa.

Katika msafara wake huo, Yanga pia imewaacha Amissi Tambwe, Yohana Nko­mola, Donald Ngoma, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ na Thabani Kamusoko ambao ni majeruhi.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad