Yametimia!...Wastara Kesho Kwenda India kwa Matibabu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Yametimia!...Wastara Kesho Kwenda India kwa Matibabu
BAADA ya kuandika habari yake kwa mara ya kwanza akiomba msaada wa matibabu ya mguu wake, hatimaye staa wa filamu Bongo, Wastara Juma amekamilisha kiasi cha shilingi milioni 37 alizokuwa akihitaji na kesho (Jumapili) anatarajia kuondoka nchini kuelekea kwenye Hospitali ya Sefaree iliyopo India kwa matibabu.

Wastara alisema kuwa, hakutarajia muitikio mkubwa wa kuchangiwa fedha hizo na anawashukuru wote waliofanikisha kupatikana kwa msaada huo.

“Niwashukuru Watanzania wote kwa kunichangia, nimshukuru Rais Magufuli na mkewe mama Janeth lakini kwa kipekee kabisa naomba nilishukuru gazeti lenu (Risasi Jumamosi) kwa kuwafanya watu wengine wajue nina tatizo gani na nahitaji msaada, bila nyie huenda mpaka leo ningekuwa nalia kitandani, asanteni na Mungu awabariki,” alisema Wastara.

Mbali na kulishukuru gazeti hili, Wastara pia ameishukuru Global TV Online ambayo ilirusha sauti yake na video ikionesha jinsi alivyokuwa akipata maumivu.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad