AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA
Zitto Kabwe amesema hayo leo Februari 24, 2018 akiongea na waandishi wa habari na kusema kuwa kitendo cha yeye kukamatwa na kulazwa ndani kwa siku moja kumemfanya agundue kuwa kuna Watanzania wengi wanateseka na kupata shida kwenye vituo vya polisi nchini.
"Watanzania wanateseka sana chini ya mikono ya polisi, sheria inataka ndani ya masaa 48 polisi wame wamewafikisha mahakamani watuhumiwa lakini tumekutana na watu wamekaa ndani siku 3 hata maelezo tu hawajaandika, wengine wana siku 20 wapo ndani hawajafikishwa mahakamani" alisema Zitto Kabwe
Kiongozi huyo aliendelea kudai kuwa polisi wamekuwa wakiwatesa wananchi ndani ya vituo hivyo vya polisi na kusababisha majeraha kwa baadhi ya watuhumiwa bila kuwapeleka hospitali kwa matibabu.
"Tumekuta watu ambao wanateswa, kijana mmoja mpaka mbavu zimevunjika na zaidi ya siku saba hajapelekwa hospitali kwa matibabu, mpaka jana tunaondoka hajapelekwa hospitali, tulipozungumza na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro tulimweleza hilo, kuna watu ni wagonjwa hawajapelekwa hospitali akasema atashughulikia sasa sijui kama yeye alikuwa hajui hilo" alisema Zitto Kabwe
Mbali na hilo Zitto Kabwe amesema hali kiujumla ya nchi yetu kwa sasa ni tata kwa kuwa suala la mauaji yameendelea kutokea kinyume na mazoea yaliyokuwepo kipindi cha nyuma na kudai kuwa kuna kila sababu ya uchunguzi wa mauaji hayo kuanzia yale ya Kibiti mpaka haya ambayo yanaendelea sasa kuchunguzwa na vyombo huru na si jeshi la polisi kwa kuwa jeshi hilo nalo linatuhumiwa.
Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.
Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA
Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.
NAFASI ZA AJIRA
JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA
GOODLUCK
Angry Face.... Jito Zumbli Kambwe kwa mara nyingine tena ameenda Ziarani huko Lupango na Kuibua mapya.
ReplyDeleteZito Zumbli Kambwe Kwa sasa anaingilia Jimbo ya Godilesi na Mtowe kiuchokozi ili aamshw lingine.
Dogo ofisi unayo au Playstation haina Chaji baada ya Luku kukatwa????
Luzuku mtowe anachukua ila kwa sasa itabidi alipie usababishaji wa Akwilina na Matokeo yake.