Zitto Kabwe Amuwakia Waziri Mpango

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Zitto Kabwe Amuwakia Waziri Mpango
Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo Mhe. Zitto Kabwe amefunguka na kusema kuwa deni la taifa limeweza kuongezeka kwa asilimia 168% ndani ya muda mfupi toka Serikali ya awamu ya tano imeingia madarakani.


Zitto Kabwe amesema hayo Januari 1, 2018 wakati akichangia Bungeni na kudai kuwa kwa mujibu wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Musa Juma Assad ndani ya kipindi kifupi deni la taifa limeongezeka.

"Ukitizama aliyosema CAG kuhusu deni la taifa inaonyesha kwamba ndani ya kipindi kifupi sana deni la Taifa limeongezeka kwa asilimia 168% lakini baya zaidi deni ambalo linatokana na masharti ya biashara limeongezeka kwa asilimia 17 ndani ya mwaka mmoja, madeni yanayotokana na masharti ya biashara gharama zake ni kubwa sana na inawezekana uwezo wetu wa kuyalipa ukawa na matatizo makubwa sana. Ndani ya taarifa hii ya CAG inaonesha kwamba taarifa ambayo Serikali ilitoa kuhusu deni la Taifa, deni la jumla ya tilioni 3.2 halikuwepo kwenye taarifa ya deni la Taifa, tulitarajia leo tungepata maelezo kwanini tilioni 3.2 hazikuhusisha katika taarifa ya pamoja ya deni la Taifa" alisema Zitto Kabwe

Mbali na hilo Zitto Kabwe alimjia juu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango na Naibu wake kwa kitendo cha kuwadanganya wananchii juu ya ujenzi wa reli mpya wa kisasa Standard Gauge kwa kusema inajengwa kwa fedha za ndani ili hali Serikali inakopa fedha ili kujenga reli hiyo.

"Serikali imekamilisha majadiliano na taasisi za kifedha kwa lengo la kukopa kiasi cha dollar za Marekani Bilioni 1.5 kwa ajili ya kugharamia ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha 'standard gauge' kutoka Morogoro hadi Makutopora Serikali inakamilisha utaratibu wa kusaini mkataba. Waziri Mpango ruhusa uliyopewa na Bunge ni kukopa dollar za Marekani Milioni 700 ni wapi ulipata ruhusa ya kwenda kujadiliana kukopa ziada ya 1.5 Bilioni ?

Zitto Kabwe aliendelea kuhoji

"Wabunge wote humu ndani ni mashahidi kila siku tunaambiwa, tunajenga reli ya Standa gauge kwa fedha zetu za ndani lakini leo Serikali inasema tunakopa, Kwanini tunawalaghai wananchi? Kwanini hatuwaelezi wananchi ukweli kwamba hatuna uwezo wa kujenga kwa fedha za ndani lakini tunakopa, kuna ubaya gani maanake kukupa si dhambi, kwanini tunamuacha Rais anasema tunajenga reli kwa fedha zetu za ndani halafu tunakuja Bungeni taarifa za Serikali zinasema kwamba tunakopa mnamuaibisha Rais" alisisitiza Zitto Kabwe 
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. We Zito Kabwe bure hali mavi ya paka afadhali. Unajipa uwezo wa kujadili mambo mazito ya Taifa na ya kimataifa wakati huna uwezo wa kusimamia hata mambo madogo madogo tu yako wewe binafsi. Nyumba yako ile iliteketea kizembe kabisa kwa moto kule kigoma. Chama cha Act wazalendo kinakufa na ni miongoni mwa vyama vinavyojiendesha kwa ruzuku. Tulitegemea Zito aoneshe uwezo wake kwa vitendo ili kukipa Act wazalendo nguvu za kiuchumi katika kubuni miradi mbali ya kiuchumi lakini hali ni hovyo kabisa. Ni tabia ya kipuuzi ya kudakia mamabo ya mbali wakati ukiayaacha ya kwako ukishindwa kuyasimamia. Ni kujitafutia umaarufu wa kipumbavu usio na na tija isipokuwa sifa za kijinga.

    ReplyDelete

Top Post Ad