Zuma Kufuata Nyayo za Mugabe Akubali Kujiuzulu Atoa Sharti Hili

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Zuma Kufuata Nyayo za Mugabe Akubali Kujiuzulu Atoa Sharti Hili
RAIS wa Afrika Kusini, Jacob Zuma ameridhia kuondoka madarakani, baada ya wito uliotolewa na Chama chake tawala cha ANC kumtaka kujiuzulu ndani ya masaa 48. Zuma ameridhia kujiuzulu kwa sharti kwamba, atafanya hivyo baada ya miezi mitatu hadi sita kuanzia sasa, ambapo bado uongozi wa ANC haujatoa jibu iwapo umeridhia sharti

ANC kikiongozwa na Cyril Ramaphosa, jana kilituma ujumbe maalum kumtaka rais huyo kuachia madaraka, kutokana na harakati nyingi za kumtaka afanye hivyo tangu mwaka jana.


Jacob Zuma anakabiliwa na tuhuma za rushwa na matumizi mabaya ya madaraka ambapo Bunge la nchi hiyo kujaribu kupiga kura za maoni ili kumuondoa lakini ilishindikana, ndipo chama kikafanya mkutano na kuchukua uamuzi huo mgumu wa kumtaka afanye hivyo, la sivyo kitamtoa kwa nguvu.


Endapo Zuma atafanya hivyo atakuwa amefuata nyayo alizopita rafiki yake mkubwa Robert Mugabe ambaye alikuwa Rais wa Zimbabwe, aliyetakiwa kufanya hivyo mwishoni mwa mwaka 2017 na jeshi la nchi hiyo, la sivyo lingetumia nguvu kumng’oa, na hatimaye kuachia madaraka.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad