AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA
Mtangazaji maarufu wa kituo cha Clouds FM, Diva The Bawse amedai kuwa baada ya kumwagana na aliyekuwa Boyfriend wake Heri Muziki amekuwa akipata usumbufu kutoka kwa wanaume hadi inakuwa kero.
Akifunguka kwenye mahojiano yake na Bongo5, Diva amesema kupitia simu yake ya mkononi amekuwa akipata meseji zaidi ya 2,000 na zote kutoka kwa wanaume wengi wakimtongoza, kitu ambacho kila mwezi kinamfanya abadilishe laini zake mara saba.
“Maisha ya kuwa single ni mazuri ingawaje nimekuwa nikipata usumbufu mkubwa kwenye simu yangu yaani napata meseji zaidi ya 2,000 na zote kutoka kwa wanaume, kitu ambacho kinanipa wakati mgumu kwani wananifanya nibadili laini mara saba kwa mwezi,“amesema Diva.
Mbali na usumbufu huo, Diva amesema kuwa kwenye ukurasa wake wa Instagram pia amekuwa akikumbana na usumbufu kama huo DM.
Kwa sasa mrembo huyo amesema kuwa ameshapata mwanaume ambaye ndiye anaamini kuwa atakuwa baba watoto wake siku za usoni ingawaje amekataa kumuweka wazi kwa sasa.
Kwa upande mwingine Diva ametangaza kuachia albamu yake mwaka huu ya ‘ALA ZA ROHO’ ambayo itakuwa na mastaa kibao kutoka nje ya nchini
Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.
Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA
Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.
NAFASI ZA AJIRA
JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA
GOODLUCK