Khadija Khopa Achoka Kuwa Single Ataka Mwanaume wa Kumuoa "Nataka Mume Sipendi Dhambi"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Khadija Khopa Achoka Kuwa Singo Ataka Mwanaume wa Kumuoa "Nataka Mume Sipendi Dhambi"Malkia wa Mipasho nchini Tanzania asiyekuwa na mshindani, Khadija Kopa ametangaza rasmi kuhitaji mume wa kumuoa ili aweze kuishi naye huku akiweka vigezo vyake kuwa hataki aliyechini ya miaka 40 kwa madai hawezi kufundisha tution.


Khadija Kopa ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa mubashara kupitia kurasa za EATV kila siku ya Jumatano kuanzia saa 8:00 mchana hadi 10:00 alasiri.

"Sijaolewa ila sitaki kusomesha tuition, nataka mwanaume aliyekuwa na umri mkubwa kuanzia 40 kwenda juu, mwenye mapenzi ya dhati na huba, mwenye kujali na kujua ninataka nini, atakayeweza kuijali familia yangu pamoja na watoto wangu, awe mnene kidogo na sio mwembamba, awe na rangi yeyote na kabila lolote lile kwasababu mimi sina ubaguzi katika vitu hivyo", amesema Khadija Kopa.

Pamoja na hayo, Khadija Kopa ameendelea kwa kusema "napenda mwanaume mfanyakazi maana kupata pesa ni majaliwa ila asiwe mwanaume wa kulala nyumbani akanitegemea mimi nikafanye kazi ili yeye aje kula maana maisha ni kusaidia nasio kuegemea upande mmoja tena wa mwanamke".

Aidha, Khadija Kopa amesema sababu kubwa iliyompelekea mpaka sasa kutoolewa ndoa nyingine baada ya aliyekuwa mume wake kufariki ni kutokana na kuwa na wasiwasi na wanaume wa sasa.

"Nina wasiwasi kwa mwanaume atakayekuja kunioa kwa sasa, maana najiuliza mengi je atakuwa na huba kama marehemu mume wangu ndio maana mpaka sasa sijaolewa kwa kuwa nafikiria sana. Mume wangu aliyefariki alikuwa ni mwenye huba, mwenye kunijali, nimekaa naye miaka yote sijawahi kugombana naye, nilikuwa natamani kumuona akinuna ananuna vipi, alikuwa na vigezo vyote", amesisitiza Khadija Kopa.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Dada hadija kweli dhambi hafai. Na pengine soul tie na marehemu mwenzi wako sijui km ungependa kupata counseling kabla ya kuolewa tena, maana inaonyesha mlishibana sana. Counselling pengine takusaidia ku-cope kwenye uhusiano. Moyai. Naamini unaweza kumpata mwenye nia km yako. Na mwingine tena juzijuzi tu naye alisema yako single na kuna elements somehow kimaelezo zinazoelekeana. Pengine ujumbe ushamfikia. Km si yeye basi Naamini mwingine atakuwepo tu.

    ReplyDelete
  2. Kweli soul tie ni pale unapojikuta kumuhitaji mwenzi wako ambaye labda ametangulia au hampo pamoja tena. Hata ukijaliwa kupata mwingine bado unamwona si kama yule wa kwanza. Counselling inaweza kutatua hilo ili kukufanya uufurahie uhusiano mpya.

    ReplyDelete

Top Post Ad