Maafisa wa Polisi Nchini Kenya Kuacha Kazi kwa Kupunguziwa Mshahara

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Maafisa wa Polisi Nchini Kenya Kuacha Kazi kwa Kupunguziwa Mshahara
Maafisa waliomaliza masomo na walemavu wameanza kuacha nafasi mbalimbali baada ya Tume ya taifa ya huduma za Polisi kupunguza mishahara yao kwa kiwango cha asilimia 50 juma lililopita.

Maafisa hao ambao tayari wamepokea mishahara yao ya mwezi Machi, wameliambia gazeti la The Nation la Jumapili kuwa, fedha zao zilikuwa zimepunguzwa, kwa wengine mpaka Sh26,000 za Kenya.

Mabadiliko hayo yaliyowaathiri polisi walioanza kazi na walemavu yamefanyika mwezi huu, ingawa amri ilitolewa na Mahakama ikielekeza serikali kutotekeleza mpango huo .

Sheria inawasamehe kodi walio na ulemavu wanaopokea mshahara wa shilingi za Kenya 150,000 na pungufu ya kiasi hicho.

Ujumbe unaoingia kwenye simu za maafisa unaonyesha kuwa baadhi yao wanapata kiasi kidogo cha mpaka shilingi 20 mwezi huu huku wengine wakiwa hawaambuliwi chochote.

Suala hilo limewaudhi maafisa huku baadhi yao wakiwa tayari wameandika barua za kuacha kazi.

Mwenyekiti wa Tume ya Huduma kwa polisi Bw Johnstone Kavuludi amekanusha ripoti hiyo na kusema kwamba hakuna afisa aliyekatwa wala kupunguziwa mshahara.


Bw Kavuludi amewaambia wanahabari kwamba kilichofanywa ni kuhakikisha kila afisa anapokea mshahara unaostahili.

"Kuna maafisa ambao hawajawasilisha vyeti vya kuhitimu stashahada na shahada lakini wanapokea mshahara wa afisa wa cheo cha konstebo, hao ndio tunapambana nao," akasema.

Tume ya Kitaifa ya Kutetea Haki za Binadamu, (KNCHR) Jumatatu imeshutumu vikali hatua hiyo ya kupunguzwa kwa mishahara hiyo ya maafisa wa polisi.

Mwenyekiti wa tume hiyo Bi Kagwira Mbogori amesema idara ya polisi imekuwa ikitekeleza majukumu muhimu ya kudumisha amani na hatua hiyo itaathiri mno mageuzi ambayo yamekuwa yakiendelezwa na tume ya huduma kwa polisi.

"Sisi tunaangazia haki za maafisa hao jinsi tunavyoshughulikia raia wanaodhulumiwa. Kwa sasa tuna kesi kadhaa ambazo tunafuatilia kuhusu raia waliowavamia polisi kipindi cha kabla na baada ya uchaguzi," amesema, kwa mujibu wa gazeti la Taifa Leo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad