MAAJABU: Mbwa azaliwa akiwa na Miguu 8 na Mikia 3

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Wakazi wa kijiji cha Mbaya, Kenya katika  eneo Lugari walipigwa na butwaa baada ya kumuona mbwa akizaa kitoto chenye miguu minane badala ya minne na mikia mitatu badala ya mmoja.

Josphat Muthoka ambaye alikuwa mfugaji wa mbwa huyo, pia alionekana kustaajabishwa na kisa hicho baada ya kugundua usiku wa Jumatatu ya February 27, 2018 kuwa mbwa wake alikuwa amezaa kitoto chenyee ulemavu usio wa kawaida

“Nilidhani mbwa wangu amezaa watoto wengi kama kawaida lakini niliposongea karibu, niligundua kwamba kilikuwa kitoto kimoja chenye miguu 8 na mikia 3, vitoto vingine 4 vilikuwa na afya ya nzuri,” Muthoka

” Hii ni mara yangu ya tatu kumuona mbwa wangu akijifungua lakini hii imenitia wasiwasi, sijawahi kuona visanga vya aina hii,” -Muthoka

Wanakijiji walikusanyika nyumbani kwa Muthoka wakitaka kujionea maajabu hayo. Aidha kuna Bibi mmoja aliyedai kuwa kisa hicho kilikuwa ishara ya kuleta matatizo kwa Muthoka kwani sio jambo la kawaida kulingana na jamii ya Waluhya.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad