Makamu wa Rais Ampa Agizo Hili IGP Sirro

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Makamu wa Rais Ampa Agizo Hili IGP Sirro
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro kuwachukulia hatua mara moja askari polisi ambao wamekiuka maadili na taratibu za jeshi hilo katika mkoa wa Kusini Pemba.

Makamu wa Rais ameyasema hayo, wakati wa kuwekwa kwa jiwe la msingi wa ujenzi wa nyumba 36 za askari polisi katika eneo la Mfikiwe, wilaya ya Chake Chake mkoa wa Kusini Pemba.

Makamu wa Rais alitoa pongezi kwa Jeshi la Polisi nchini kwa kuhakikisha nchi inakuwa tulivu na yenye amani pia alitoa pongezi kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Hamad Masauni kwa kusimamia vyema zoezi la ujengaji nyumba za Polisi.

Makamu wa Rais pia alitoa pongezi kwa kampuni ya Twiga Cement kwa kutoa Saruji mifuko zaidi ya elfu sita pamoja na kampuni za Shubash Patel kwa kuchangia vifaavingine vya ujenzi.

Awali Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Nchini, Mhandisi Hamad Masauni alipongeza Jeshi la Polisi kwa kupambana na biashara haramu ya madawa ya kulevya na kusema yeyote atakayevunja sheria achukuliwe hatua bila kujali wadhifa au umaarufu wake.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad