Msinifananishe na Alikiba Bado Sijamfikia Hatua Aliyokuwa Nayo- Aslay

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Msanii wa BongoFleva anayefanya vizuri na kibao chake cha 'SabalKheri Mpenzi' alichoshirikiana na Nandy, Aslay amewataka mashabiki zake kuacha kumlinganisha yeye na mkongwe Alikiba kwa madai bado hajaweza kufika hatua aliyokuwa nayo Kiba.


Aslay ametoa kauli hiyo baada ya kupita kipindi kirefu kwa baadhi ya mashabiki kudai uwezo aliokuwa nao kwa sasa  anaweza hata akamfunika Alikiba pindi wakiamua kufanya 'show' ya pamoja au hata wakiandaa tamasha siku moja basi watu wengi wataenda kwa Aslay.

"Kama kuna mashabiki wanafanya kitu kama hicho wanakosea kabisa tena sio vizuri, kwa maana hao wameshafika katika level zingine, na mimi ninajitahidi nifike huko siku moja. Kwa hiyo ukinishindanisha kwanza utaniua kisaikolojia kwasababu nitajiona na mimi nimeshafikia hatua zao kumbe bado sana", amesema Aslay.

Pamoja na hayo, Aslay ameendelea kwa kusema "ukisema umlinganishe Aslay na Alikiba utakuta kuna vitu vingi vinakukosoa kwsababu yeye ameshaingia katika Tuzo mbalimbali kubwa mpaka kufika sasa hivi na hata akifanya 'show' anajaza watu kwa hiyo mimi naona sio watu wa kushindana nao sasa hivi".

Kwa upande mwingine, Aslay amesema muda huu kwake sio wa kushindana na wasanii waliyomzidi ufanisi na uwezo wa kimuziki bali anajikita zaidi katika kujiboresha ili nae siku afike walipofika wanamuziki wakubwa waliopo nchini Tanzania.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad