Mwanasheria Miguna Miguna Akataliwa Kuingia Kenya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mwanasheria wa upande wa upinzani wa Kenya,Miguna Miguna amekataliwa kuingia Kenya baada ya kukataa kuomba Visa, gazeti binafsi la The Star la ripoti.

Bwana Miguna anasafiri kwa kutumia kibali chake cha kusafiria cha Canada baada ya kuvuliwa uraia wa Kenya.

Mamlaka ya Kenya ilimrudisha Canada baada ya kushiriki katika kuapishwa kwa kiongozi wa upinzani Raila Odinga kama "Rais wa watu".

Wiki iliyopita Miguna aliiambia BBC kuwa mamlaka ya Kenya haijafuata maagizo ya mahakama ya kumpatia hati za kusafiria za Kenya.

Serikali ya Kenya ilimvua uraia Miguna na kumrudisha Canada ambapo pia ni raia huko.

Mahakama ya kenya ilitoa amri kwa serikali hiyo kurudisha hati za kusafiria za Miguna na kusaidia katika kurejea kwake lakini kwa mujibu wa Miguna serikali haija fanya hivyo.

Mwandishi wa BBC Ferdinand Omondi ambaye alikwenda katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta amesema vyanzo vinasema serikali inataka kumpa visa ya muda wa miezi sita na kuchukua pasipoti yake.

Waandishi wa habari wa Kenya wamekusanyika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta uliopo Nairobi, ili kupata taarifa ya ujio wa wakili huyo wa upinzani Miguna Miguna ambaye aliondolewa Kenya tangu tarehe 6 mwezi Februari mwaka huu.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad