Napitia Maisha Magumu Katika Muziki Ndomana Nashindwa Kufanya Vizuri- Enock Bella

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Napitia Maisha Magumu Katika Muziki Ndomana Nashindwa Kufanya Vizuri- Enock Bella
Msanii wa BongoFleva Enock Bella amedai anapitia wakati mgumu katika muziki kwa sasa ndio maana anashindwa kufanya vizuri katika kazi zake kwa maana kila jambo analisimamia yeye binafsi hakuna wa kumpa ushirikiano kwa jambo lolote lile.


Enock amebainisha hayo kupitia kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya msanii huyo kuonekana kutoa nyimbo tano lakini bado anaonekana kususua sua tofauti na wenzake aliyekuwa nao kwenye kundi la Yamoto Bendi wakiendelea kufanya vizuri ndani na nje ya mipaka ya Tanzania huku baadhi ya watu wakidai kutofanikiwa kwa Enock ni kutokana na sauti yake aliyokuwa nayo tofauti na wenzake.

"Kila kitu kina sababu yake na Mungu pekee ndiye mwenye kujua nafasi ya mtu wapi ilipo kwa hiyo siwezi kulazimisha muda huo huo ninaotoa wimbo na nipate mafanikio hapo hapo, kila mtu ana nafasi yake aliyeba katika maisha yake. Muda wangu utakapofikia mtaoana maendeleo ya kimuziki ambao mimi nafanya kwa maana kuna watu wengine wametajirika wakiwa wazee, muda waliokuwa vijana hawakufanikiwa kupata mafanikio yeyote yale", amesema Enock.

Pamoja na hayo, Enock Bella ameendelea kwa kusema "ridhiki ni mafungu saba lakini sasa hivi imekuwa ni mambo mawili ambayo ni kupata na kukosa kwa hiyo wakati wangu ukifika nami ntakuwa nimeanzia hapo kufanikiwa. Sauti ya yangu hii ya 'base' ndio iliyonitengeneza mimi hii leo kutambulika hivyo sio kweli kwamba sauti yangu ndio sababu ya hayo, kwa hiyo nikisema ghafla niipoteze halafu niambie upande mwingine itakuwa ni tofauti ndio maana nikasema kila mtu ana nafasi yake hivyo nafasi yangu ikifika kwa 'base' yangu hii hii watarudi tu. Kwani mara ya kwanza waliokuwa wananielewa nilivyokuwa kwenye Yamoto ?, si walikuja kunielewa baada ya mashairi yangu kuyatoa".
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad