Wafuasi wa Chadema Wafurika Mahakamani Kusikiliza Dhamana ya Viongozi wa Chadema Ulinzi Wahimarishwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wafuasi wa Chadema Wafurika Mahakamani  Kusikiliza Dhamana ya Viongozi wa Chadema  Ulinzi Wahimarishwa
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limeimarisha ulinzi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ili kudhibiti umati wa watu wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambao wamekusanyika nje ya mahakama, wasiingie kusikiliza kesi inayowakabili mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe na viongozi wenzake watano.


Mbowe na wenzake wameshafikishwa mahakamani hapo wakitokea mahabusu ya Segerea wakikabiliwa na mashtaka manane yakiwemo kufanya maandamano yaliyosababisha kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline, Februari 16, mwaka huu, uasi na kuhamasisha chuki.


Wabunge wa Chadema, wafuasi na wananchi wengine wakiwa mahakamani kufuatilia kesi hiyo.

Baadhi ya wabunge wa Chadema, wafuasi wa chama hicho na wananchi wengine waliofika mahakamani kufuatilia kesi hiyo ni  Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Prof. Abdallah Safari, Mbunge Joseph Haule ‘Prof. Jay.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad