Watumishi Watano wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Wafikishwa Mahakamani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU imewafikisha mahakamani Wafanyakazi watano wa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro  kwa kosa la kuisababishia hasara serikali  dola za Kimarekani 35,500.

Watuhumiwa ni pamoja na Joseph Mtwala{36},John Mlambo{42},Mwahu Yunus {38},Mery Njau{38} na Catherini Edward {33}.

Watuhumiwa hao wote kwa pamoja walisomewa shitaka moja na Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa{TAKUKURU} ,Adamu Kilongozi akiwa na Hamidu Simbano na Richard Jacopiyo kuwa walitenda kosa hilo kati ya desemba 25 mwaka 2013 na juni 6 mwaka 2014.

Kilongozi alidai mahakamani hapo kuwa watuhumiwa hao wakiwa katika lango la Nabi Mkoani Mara na lango kuu la Loduare Mkoani Arusha watuhumiwa hao walisababishia serikali hasara ya fedha za Kimarekani kiasi hicho wakiwa watumishi wa NCAA.

Mwendesha mashitaka huyo alisoma shitaka hilo mbele ya Hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha,Bernad Nganga na kueleza kuwa walifanya kosa hilo huku wakijua ni kinyume na sheria.

Watuhumiwa wote walikana shitaka hilo na walipewa dhamana ya fedha taslimu shilingi milioni 7.9 au mali isiyohamishika yenye thamani hiyo na taratibu za dhamana zilikuwa zikiendelea .

Mwendesha mashitaka wa TAKUKURU alisema kuwa ushahidi wa kesi hiyo umekamilika na aliiomba mahakama hiyo kupanga Tarehe ya kuanza usikilzwaji wa awali.

Watuhumiwa wote watano wamepelekwa rumande kwakushindwa kukidhi masharti ya dhamani ,ambapo watasomewa hoja za  awali April 10 mwaka huu.

Na Ferdinand Shayo,Arusha.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad