Mahakama Yamkuta na Kesi ya Kujibu Wema Sepetu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mahakama Yamkuta na Kesi ya Kujibu Wema SepetuMahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema msanii Wema Sepetu na wafanyakazi wake wanaokabiliwa na tuhuma za kutumia dawa za kulevya wana kesi ya kujibu, hivyo wataanza kujitetea.
Uamuzi huo, umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya wakili wa serikali, Constantine Kakula kuele
za kuwa kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya uamuzi kama washtakiwa wana kesi ya kujibu ama lah.
Katika uamuzi wake Hakimu Simba amesema kwa mujibu wa sheria kama washtakiwa wakipatikana na kesi ya kujibu watatakiwa kujitetea, pia kama hawana kesi ya kujibu wataachiwa huru.
“Baada ya kupitia hoja zote, mahakama imejitosheleza kwamba washtakiwa wote wana kesi ya kujibu katika mashtaka yote, hivyo wana haki kisheria kuanza kujitetea,” amesema Hakimu Simba.
Baada ya kusema hayo, Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi May 14 na 15,2018 ambapo washtakiwa watajitetea mfululizo.
March 23,2018 upande wa utetezi kupitia wakili Alberto Msando, uliwasilisha hoja katika mahakama hiyo kwamba washtakiwa hawana kesi ya kujibu.
Mbali na Wema washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ya kutumia dawa za kulevya ni Angelina Msigwa  na Matrida Seleman Abbas.
Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya.
Inadaiwa kuwa February 4,2017 katika Makazi ya Wema huko Kunduchi Ununio  washtakiwa hao walikutwa na msokoto mmoja na vipisi vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08.
Kwa upande wa Wema yeye anadaiwa kuwa February Mosi, 2017 katika  eneo lisilojulikana jijini Dar es Salaam, alitumia dawa za kulevya aina ya Bangi.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad