Polisi Watoa Password ya Simu kwa Kutumia Kidole cha Marehemu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Polisi Watoa Password ya Simu kwa Kutumia Kidole cha Marehemu
Kutoka Florida nchini Marekani, Jeshi la Polisi limeshukiwa na watu baada ya askari polisi wawili kuingia kwenye nyumba iliyokuwa na msiba na kushinikiza kufungua ‘unclock‘ simu ya marehemu.

Inaelezwa kuwa marehemu huyo Linus Phillip, 30, aliuawa pindi alipojaribu kuwatoroka polisi katika kituo cha mafuta eneo la Largo mnamo March 23, 2018.

Baada ya mwili wake kuachiwa na polisi kwa ajili ya mazishi, wanafamilia wameeleza kuwa waliingia maaskari wawili ambao walijaribu kutumia vidole vya marehemu ili kufungua simu yake.
Mpenzi wa marehemu Victoria Armstrong ameeleza kusikitishwa na kitendo hicho ambacho polisi wenyewe wamedai kuwa ni sehemu ya upelelezi wao.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Top Post Ad