AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA
MSANII wa muziki wa dansi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Werrason yupo nchini Tanzania kwa ajili ya kufanya shoo Jumamosi hii katika fukwe za Escape One Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Muda mfupi uliopita mwanamuziki huyo alipata fursa ya kuzungumza na waandishi wa habari katika kikao kilichofanyika katika fukwe hizo ambapo amesema hapa nchini anamfahamu Msanii Diamond Platnumz pekee maana amekuwa akimsikia mara kadhaa akitajwa huko Congo.
Werrason na wanamuziki wake wakitoa kionjo cha wimbo kabla ya kuhitimisha kikao na wanahabari.
Hivyo amewaomba wasanii wa hapa nchini wamtafute kuanzia leo ili wabadilishane mawazo na hata ikiwezekana kufanya klabo ya pamoja kabla ya siku yake ya kufanya shoo yake hiyo ya Jumamosi na ile ya Jumanne katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Waandishi wa habari wakichukua matukio mbalimbali ya kikao hicho kilichofanyika katika fukwe za Escape One mapema leo.
“Waafrika ni kitu kimoja hivyo ningependa wiki hii moja ambayo nipo hapa nipate kubadilishana mawazo na wasanii wa hapa Tanzania, ila hata kama kuna mtu angependa tufanye ngoma ya pamoja nipo tayari kwani kufanya hivyo ni kukuza muziki wetu wa Afrika ambapo utapata promo ya nchi nyingi jirani,” alisema Werrason.
Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu
Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:
NAFASI ZA AJIRA
JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA
GOODLUCK
ni msanii mkali sana Congo natamani ningekuwa bongo ningeenda kwenye show kumuangalia anazo video kali sana huwa naziangalia
ReplyDelete