Bunge Laahirisha Vikao vya Bunge Kuomboleza Kifo cha Mbunge...... Chadema Watoa Ratiba Hii ya Kuaga Mwili

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Bunge Laahirisha Vikaovya Bunge Kuomboleza Kifo cha Mbunge...... Chadema Watoa Ratiba Hii ya Kuaga Mwili
Naibu Spika wa Bunge Dr Tulia Ackson leo May 28, 2018 ameahirisha Bunge mpaka kesho saa 3 asubuhi kupisha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Kasuku Bilago aliyefariki Jumamosi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Mwili wa marehemu unatarajiwa kuagwa bungeni kesho Jumanne kuanzia saa 6 mchana, na kuzikwa jimboni kwake Jumatano.

Hii hapa Ratiba ya kuuaga na kumzika marehemhu Kasuku Bilango:

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa rasmi ratiba ya kuuaga na kumzika marehemhu Kasuku Bilango aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Buyungu mkoani Kigoma ambaye amefariki mwishoni mwa juma lililoisha katika Hospitali ya Taifa Muhimbili akipatiwa matibabu.


Ratiba hiyo imewekwa wazi na Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje ya CHADEMA, John Mrema na kusema baada ya kikao kilichokaliwa baina ya familia na viongozi wakuu wa chama hicho Mei 27, 2018 walikubaliana siku ya leo kufanyike ibada fupi na kuuaga mwili katika viwanja vya Karemjee Jijini Dar es Salaam majira ya saa sita mchana na mwishowe mwili huo kupelekwa uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa ajili ya kupelekwa Bungeni Jijini Dodoma ili wabunge wapate kuuaga siku ya kesho katika viwanja vya Bunge.

Aidha, Mrema amesema baada ya zoezi hilo kukamilika kwa Wabunge mwili wa marehemu Kasuku utasafirishwa kwa ndege kuelekea Kibondo ambapo itakapofikia siku ya Jumatano Mei 30 wananchi wa Jimbo la Buyungu watapata fursa ya kuuga mwili katika eneo ambalo litatangazwa baadae.

"Mei 31 ndio siku ya mazishi rasmi ambayo yatafanyika nyumbani kwa marehemu huko Wilayani Kakonko, Kigoma. Tunatoa wito kwa wanachama, wapenzi na watanzania wote tuendelee kuikumbuka familia ya marehemu katika sala na dua katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao ili Mungu aendelee kuwapa faraja",imesema taarifa hiyo.

Enzi za uhai wake Mhe. Kasuku Bilango alikuwa Mbunge wa Jimbo la Buyungu, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Magharibi yenye Mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad