Kama Unataka Kufurahia Mapenzi oa Mwanamke Asiye na Kazi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Wanawake wasio na Kazi wanakua hawana mambo mengi. Ukitoka kwenye mihangaiko yako anakupokea na kukukaribisha Nyumbani kwa furaha. Utakuta chakula kishaiva, utakuta Watoto wasafi kama mmebahatika kuwa nao, hata ukimuachia hela ya matumizi anatumia Vizuri tena unampa hela kwa furaha kabisa. Mkibahatika kupata Mtoto hutakuwa na mawazo ya Mtoto wako kupigwa na House girl. Ukitembelewa na Familia, hawataboreka kwani muda wote watakua na mwenyeji Mama mwenye Nyumba.

Jidanganye uoe Mwanamke mwenye Kazi. Asilimia kubwa wanarudi wamechoka kiasi kwamba hata mkilala hakugeukii wala hataki umguse. Atataka haki sawa eti akipika wewe ufue Nguo au umsaidie Kupika. Mara chache atakutengea Maji ya kuoga. Muda mwingi anatoka Kazini amenuna, hata akichelewa hataki umuulize alikua wapi.

Wana viburi sana, ukiwauliza kitu wanajibu kwa nyodo, hatakusikiliza. ukimsemesha kidogo tu ataenda kulala kwa marafiki zake au kwa ndugu zake. Haoni aibu kukukolomea Mwanaume hata mbele za watu. Anajifanya anawivu sana, atapiga Simu kila dakika kukuuliza ulipo as if wewe mtoto mdogo hujui pa kwenda.

Anapewa Mshahara lakini hautojua unaenda wapi kwani kila siku utaombwa hela ya Salon. Siku ukiishiwa ukamuomba hela ya Bia hatakupa bali atasema siwezi kukupa hela yangu ukahonge Malaya zako.

Siku akifurahi atakuletea zawadi ya Shati, mara moja kwa Miezi Mitano kana kwamba halipwi Mshahara. Dawasco wakimkuta hatawapa hela yake hata kama anayo, atawambia hayupo.

Ukioa Mwanamke mwenye kazi utamfaidi siku ukiumwa, ataomba ruhusa ili aje akuhudumie, atakununulia sana Socks na Matunda Matunda. akitaka kununua kitu atakua na kianzio sana sana ataomba umuongezee Hela.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad