Kuna maisha ya ustaa na kuna maisha ya kuigiza kuwa staa – Alikiba

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Msanii wa muziki Bongo, Alikiba amesema licha ya umaarufu mkubwa alionao ataendelea kuishi maisha ya kawaida ya kutojionyesha (show off).

Muimbaji huyo katika mahojiano na Dj Show ya Radio One amesema kuwa maisha anayoishi ndio anaona yanafaa zaidi machoni kwa mashabiki wake ambao walimpokea kipindi hana kitu.

“Kuna maisha ya ustaa na kuna maisha ya kawaida na kuna maisha ya kuigiza kuwa staa. Mimi sijachagua in nature nipo hivyo, Watanzania walinipokea katika hali ambayo kiukweli haisemeki sasa hii leo nije nibadilike, so nisingependa kumshawishi shabiki yangu kwa namna yoyote ile kuwa nimebadilika kwa sasa hivi,” amesema.

“Kwa hiyo ule wivu wa kumfanya mtu anze kunichukia kwamba Ali amekuwa hivi na hivi, hapana!. Mimi ni staa, mimi ni supa staa nitafanya, ninaishi maisha ambayo nimechagua lakini bado nitaendea ku-humble kwa watu,” ameongeza.

Alikiba kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la Mvumo wa Radi.

Bongo5
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huna ustaaa wowote Muha wewe rudi kwenu Kigoma,Ujiji ukachimbe mawese huko. Huna lolote lile. Staa utakuwa wewe mxeeeeeeee............Waha wavivuuuuuuu mxeeeeeee.......

    ReplyDelete

Top Post Ad