Wabunge, Mawaziri Wakatiwe Maji na Wao Waone Adha Wanayopata Wananchi- Ester Bulaya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wabunge, Mawaziri Wakatiwe Maji na Wao Waone Adha Wanayopata Wananchi- Ester Bulaya
Mbunge wa Bunda Mjini (Chadema), Ester Bulaya amesema tatizo la maji ni kubwa nchini, akipendekeza mawaziri na wabunge kukatiwa huduma hiyo ili waone adha wanayoipata wananchi.

Akichangia mjadala wa hotuba ya bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji ya mwaka 2018/19, Bulaya amesema fedha zinazotengwa hazitolewi.

Amesema leo Mei 7, 2018 kuwa, kuna hospitali zinashindwa kufanya upasuaji kwa kukosa maji, huku wanawake wakipata adha.

Mbunge huyo amesema wabunge na mawaziri wakikatiwa maji watahisi uchungu wanaopata wananchi wa kukosa maji safi na salama.

Amesema ilivyo sasa ni bora mgonjwa akapelekewa ndoo ya maji kuliko chakula.

Bulaya amesema hata vijana wanapohamasishwa kuwekeza katika kilimo cha umwagiliaji kama hakuna maji ni kazi bure.

“Tunaguswa na tatizo la Watanzania, tunaguswa na tatizo la ajira kwa vijana, ambao wanakwenda kuwekeza katika kilimo lakini hakuna maji,” amesema.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Top Post Ad