Waweza Kwenda Jela miaka 5 Ukimkonyeza Mwanamke

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Imeelezwa kuwa shambulio la aibu kwa mwanamke sio tu kupiga kelele dhidi yake au kumgusa bali hata kumkonyeza pekee ni lugha ya ishara inayoweza kukupeleka kuenda jela endapo ushahidi ukithibitika.

Mara baada ya kuibuka mjadala uliozua gumzo mitandaoni kuhusiana na shambulio la aibu dhidi ya wanawake eatv.tv ilimtafuta mwanasheria ili kupata ufafanuzi kuhusu shambulio hilo ambapo, Wakili wakujitegemea Johanes Konda amesema kwamba wanawake wengi hawatambui kama kukonyezwa bila ridhaa yao ni kosa kisheria.

"Kanuni za adhabu sura ya 16 ndio inaelezea zaidi kuhusiana na shambulio la aibu lakini kulingana na mazingira na tamaduni zilizopo sasa, dada zetu wanaona kawaida tuu lakini sheria imewekwa kwa ajili ya kuwatetea wao dhidi ya shambulio hilo ambalo linaweza kuwa ni kwa kuguswa au kwa ishara kama kukonyeza au kupiga kelele za kuashiria kuna kitu cha tofauti kimepita", amesema Wakili Konda.

Wakili Konda amesema kuwa endapo wahusika ambao ni wanawake wakizitambua haki zao na kuwashitaki watuhumiwa wanaweza kusaidia kuondoa tabia hizo na endapo ikithibitika basi adhabu yake ni kuanzia miaka isiyozidi 10 kushuka chini.

Hivi karibuni Kamanda wa Polisi wa mkoa wa mjini Magharibi Kamishna Msaidizi Mwandamizi Hassan Nassir amesema ni marufuku kukohoa pale unapopishana au unapomwona mwanamke mwenye makalio makubwa kwamba kukohoa huko kutapelekea kukamatwa kwa maana kitendo hicho ni 'shambulio la aibu”.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad