Baada ya Vifo vya Watu 10 Kigoma..... Serikali Kujenga Vizuizi Kuzuia Magari Kugonga Treni

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Baada ya Vifo vya Watu 10 Kigoma..... Serikali Kujenga Vizuizi Kuzuia Magari Kugonga Treni
Katika kudhibiti ajali katika maeneo ambayo barabara imepishana na reli, Serikali imesema itahakikisha inajenga vizuizi katika maeneo hayo ili magari yawe yanasimama wakati treni ikipita.

Hayo yameelezwa leo Ijumaa Juni 8, 2018 na mkuu wa wilaya ya Kigoma, Samson Anga ikiwa zimepita siku mbili tangu kutokea ajali ya basi dogo lililogonga treni eneo la Gungu mkoani Kigoma na kusababisha vifo vya watu 10 na wengine 35 kujeruhiwa.

“Haiwezekani watu wapoteze maisha kwa sababu ya uzembe wa baadhi ya madereva. Tumechoka kuona hali hii ikiendelea na lazima tuchukue hatua kuokoa maisha ya binadamu wenzetu," amesema.

Amesema ujenzi wa vivuko utahusisha wakala wa barabara (Tanroads) na Shirika la Reli Tanzania(TRC) ambao wataratibu na kujenga vizuizi hivyo.

Maeneo ambayo reli imepishana na barabara mkoani Kigoma ni Kibirizi, Gungu, Nyamoli, Kazuramimba, Uvinza, Tubira na Malagalasi.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad