Balozi wa Syria aiomba radhi Serikali ya Tanzania

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Balozi wa Syira nchini Abdulmonem Annan ameiomba radhi serikali ya Tanzania baada ya kusambaa kwa video iliyomuonyesha akisema atahamasisha raia wa Syria, wasiwekeze nchini kwa kile alichodai polisi hawalifanyii kazi suala la kuporwa fedha kwa Ofisa Ubalozi wa Syria.

 Machi 20, Ofisa Ubalozi huyo, Hassan Alfaouri alishambuliwa na watu wasiojulikana na kuporwa zaidi ya euro 9300(zaidi ya Sh 25 milioni).

Baada ya tukio hilo, Balozi huyo alisema  alitoa taarifa kwenye mitandao ya kijamii  kwa njia ya video akisema kuna ufuatiliaji hafifu wa suala hilo na hivyo atahamasisha raia wa Syria wasije kuwekeza nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Suleman Salehe alisema maneno aliyosema balozi Annam yalikuwa ni ya uchochezi hivyo waliamua kufanya nae mikutano minne.

Alisema wao kama Wizara walifanya jitihada na kuhakikisha jeshi la polisi linafanya uchunguzi na kuhusiana na tukio hilo na kuwakamata watu wawili ambao ni dereva na katibu wake.

“Wizara inamshukuru Balozi kufunguka na kutoa taarifa muhimu kuwa ametaarifiwa na jeshi la polisi kuwa watuhumiwa wawili wamekamatwa na sehemu ya kiasii cha fedha kimepatikana”amesema Salehe

Amesema kwa kuwa balozi amebakiza miezi michache  amalize muda wake hapa nchini, Wizara itaanda taarifa ili aweze kukutana na Mkuu wa jeshi la polisi na washughulikie suala hilo.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Top Post Ad