Hakuna Mchezaji Atakaa na Kula Pesa Tu - Simba

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Hakuna Mchezaji Atakaa na Kula Pesa Tu - Simba
Klabu ya Simba kupitia kwa kocha wake Masoud Djuma, amesema katika usajili unaofanywa na timu yake hategemei kama kutakuwa na mchezaji atasajiliwa kwaajili ya kukaa na kusubiri mshahara tu.

Masoud ameyasema hayo kwenye uwanja wa Boko Veteran jijini Dar es Salaam, ambako timu hiyo imeweka Kambi kwaajili ya maandalizi ya michuano ya Kombe la Kagame inayotarajiwa kuanza Juni 28.

''Huu mwaka tumesema hakuna mchezaji anasajiliwa Simba kuja kukaa benchi, atakaa benchi tu kwasababu kocha amefanya mabadiliko ya kikosi lakini hakuna mchezaji atakaa tu na kula mshahara, hilo hatulitaki'', amesema.

Masoud ameongeza kuwa michuano ya Klabu bingwa Afrika Mashariki na kati maarufu kama Kagame ataitumia kupima kikosi chake ili ajue naani atafaa kwenye eneo gani na endapo anakosekana mchezaji fulani asiwe na taabu kwenye kujua nani ataziba nafasi yake.

Simba ipo Kundi C  na timu za Singida United, APR ya Rwanda na Dakadaha ya Somalia. Simba itafungua dimba na timu ya Dakadaha Julai 30, Saa 10:00 jioni Uwanja wa Taifa. Hapo jana Simba imekamilisha usajili wa mshambuliaji Meddie Kagere kutoka Gor Mahia ya Kenya.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Top Post Ad